Home Habari za michezo MASHABIKI YANGA WAWAZIDI SIMBA KWA HELA….WAICHANGIA KLABU YAO BILIONI MOJA ZA USAJILI...

MASHABIKI YANGA WAWAZIDI SIMBA KWA HELA….WAICHANGIA KLABU YAO BILIONI MOJA ZA USAJILI NCHI NZIMA…


Wakati mashabiki wa Simba wakichangia klabu yao Milioni 60 toka waanze kampeni yao ya Ujenzi wa Uwanja,
Yanga imeweka wazi kwamba mchakato wa usajili wa wanachama umeiingizia klabu hiyo kiasi cha Sh1 bilioni kupitia ada za uanachama.

Mohammed Kirra Mtendaji Mkuu wa Kilinet amesema katika kipindi cha miezi sita ambayo wamekuwa wakisajili wanachama wa klabu hiyo wamefanikiwa kukusanya kiasi cha sh 1.07 bilioni.

Kirra amesema kiasi hicho kimetokana na usajili wa wanachama jumla 34,650 ambao kila mmoja amekuwa akilipa ada ya sh 29,000.

“Tumekuwa tukisafiri mikoa mbalimbali na takwimu zinaonyesha katika mkoa ambao umeongoza kwa usajili wa idadi kubwa ya wanachama ni Dar es Salaam ambao tulisajili wanachama 12124,” amesema Kirra.

“Kwa upande wa Kanda takwimu zetu zinaonyesha kwamba Pwani ndio imeongoza kwa kutupatia wanachama 15,804.

Aidha Kirra ameongeza kuwa baada ya mafanikio hayo ya eneo la usajili wa wanachama sasa wataingia katika sura nyingine ya usajili wa mashabiki ambao watakuwa wakilipa kiasi cha sh 17,000 kwa ada ya mwaka.

SOMA NA HII  MAYELE AVUNJA UKIMYA MKATABA WAKE NA YANGA...ATAJA TIMU VIGOGO AFRICA ZINAZOMTAKA.....