Kuelekea katika mchezo wa fainali ya kombe la Azam Sports (ASFC) kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa leo Jumamosi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mashabiki wa Yanga wametamba timu yao kuibuka na ushindi.
Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na rekodi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu bila kupoteza mchezo hata mmoja ikishinda 22 sare 8 na kujikusanyia pointi 74 huku la kuvutia zaidi ni kutangaza ubingwa huo mbele ya Coastal Union.
Shamir Miraji ni shabiki wa Yanga yeye anasema kikosi chake ni bora na namna ambavyo mwalimu amekiandaakikosi chake na ana asilimia zote kwamba lazima watashinda na kubeba ubingwa mwingine tena msimu huu.
Amesema wao fainali walishamaliza katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya watani wao Simba ya kesho ni sherehe tu za kukabidhiwa ubingwa wa ASFC kwani haoni wapi Coastal wanaweza kuponea katika mchezo huo.
Maulid Rashid ni Mwenyekiti wa Yanga tawi la Stendi Kuu ya mabasi Arusha anasema kama mashabiki wamejiandaa vyema kuchukua ubingwa mwingine basi hakuna namna Coastal itatoka salama katika mchezo huo.
“Yanga ni timu ambayo imedhamiria kuchukua vikombe vyote kwa msimu huu na tayari cha Ligi tunacho bado huo ambao kesho tunashinda alafu tunaendelea na Royal Tour”. amesema Maulid.
Afisa hamasa wa Yanga Mkoa wa Arusha, Ragumboz Gumbo amesema hamasa imekuwa kubwa sana kwa mashabiki kujitokeza kesho kuipa sapoti timu na kubeba ubingwa huo ambao ni imepita miaka saba bila kuibeba tangu mwaka 2016.