Dodoma Jiji imeendelea kutikisa soko la usajili baada ya kumtambulisha rasmi Striker wa Kagera Sugar, Hassan Mwaterema.
Mbali na kucheza Striker Mwaterema pia hucheza winga na kabla ya kutua Kagera Sugar aliichezea JKT Tanzania.
Mwaterema anapishana na Striker wa Dodoma Jiji, Anuary Jabir ambaye tayari amemalizana na ‘Wanankurukumbi’Kagera Sugar.
Mpaka sasa Dodoma Jiji imekamilisha usajili wa wachezaji Daniel Mgore, Collins Opare na Christian Zigah kutoka Biashara United.
Wachezaji wengine waliotambulishwa na timu hiyo ni Randy Bangala (TP Les Croyant) Amani Kyata,Rashid Chambo (Coastal Union), Peter Paul (Azam) na Jimmy Shoji (Mbeya Kwanza)
Ofisa Habari wa timu hiyo, Moses Mpunga amesema mchezaji huyo amesaini kandarasi ya miaka 2 kuwatumikia walima za zabibu hao ambao msimu uliomalizika hawakuwa na matokeo mazuri.