Home Habari za michezo KUHUSU TETESI ZA TARIMBA KUIKATAA SIMBA KWENYE DILI LA SportPesa..UKWELI WA MAMBO...

KUHUSU TETESI ZA TARIMBA KUIKATAA SIMBA KWENYE DILI LA SportPesa..UKWELI WA MAMBO UKO HIVI…


Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Saleh Ally ‘Jembe’ ametoa ufafanuzi kuhusu taarifa zinazoenea mitandaoni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa Abas Tarimba amehusika katika kukwamisha dili la Kampuni hiyo yakubashiri na Simba SC.

Jembe amesema habari hizo si za kweli licha ya kwamba Tarimba ni mwana Yanga lakini Simba waliachana na dili la SportPesa kutokana na kupata dili jingine la M- Bet.

Aidha amesisitiza kuwa Tarimba ndiyo alikuwa mtu wa kwanza kuvishawishi vilabu hivi vikubwa nchini vya Yanga na Simba kukubali udhamini wa SportPesa mwaka 2017 ili kuvisaidia viweze kujiendesha kwa mafanikio na ni katika kipindi hico ambapo Simba SC imepata mafanikio makubwa licha ya kuwa ailikuwa inapata mkataba wenye maslahi sawa na watani wao wa jadi Yanga SC.

Jana Klabu ya Yanga ilisaini mkataba na Kampuni ya Michezo ya kubashiri ya SportPesa wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 12 za kitanzania ambao utadumu kwa muda wa miaka mitatu (3).

SOMA NA HII  RASMI...MORRISON ARUDI ZAKE YANGA...APEWA MSHAHARA WA CHAMA..MKATABA WAKE KUFURU..SIMBA WAITANA FASTA..