Home Habari za michezo MFAUME : YANGA HAINA THAMANI YA KUPATA MKATABA MNONO KAMA WA SportPesa…USHABIKI...

MFAUME : YANGA HAINA THAMANI YA KUPATA MKATABA MNONO KAMA WA SportPesa…USHABIKI WA TARIMBA UMECHANGIA…


Mchambuzi wa Soka, Mfaume Nalinga ametoa maoni yake juu ya Mkataba ulioingia klabu ya Yanga na SportPesa huku akibainisha kuwa klabu ya Yanga haikustahili kupata dili hilo kwani haina thamani hiyo.

Amebainisha kuwa uwepo wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa ambaye ni shabiki na Mwanachama wa klabu ya Yanga Abbas Tarimba umechochea suala hilo kupelekwa kishabiki na Yanga kupata dili ambalo lina thamani kubwa kuliko thamani halisi ya klabu hiyo.

Jana klabu ya Yanga iliingia mkataba na Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa wenye thamani ya Bilioni 12.033 kwa kipindi cha miaka mitatu (3) ambao utakuwa na mchanganuo wa kuipatia klabu ya Yanga kiasi cha shilingi Bilioni 4 kila mwaka.

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA WAKISIMAMIA UKUCHA KWENYE JEZI ZAO...YANGA WAKUBALI KUSHUKA...MANARA IBUKA NA KAULI HII...