Home Azam FC BAADA YA AZAM FC KUMUACHA NA KUMUANIKA MITANDAONI…MUDATHIR AVUNJA UKIMYA…AIBUKA NA HILI...

BAADA YA AZAM FC KUMUACHA NA KUMUANIKA MITANDAONI…MUDATHIR AVUNJA UKIMYA…AIBUKA NA HILI JIPYA…

                                                                                           


Ikiwa ni siku kadhaa baada ya kuachwa na Azam FC, kiungo Mudathir Yahya amesema bado ana nafasi ya kucheza timu yoyote anayotaka kucheza hivyo hana wasiwasi ni suala la muda tu kufahamu ni wapi atacheza msimu ujao.

Mudathiri ambaye ameichezea Azam miaka 11 alisema; β€œNimekaa Azam muda mrefu na nimecheza kwa kujitolea, naushukuru uongozi kwa kuniamini na kunipa nafasi ya kuwatumikia kwa misimu mingi zaidi, ni muda wangu sasa kwenda kujaribu maisha mengine nje ya timu niliyoizoea,” amesema Mudathir.

Alisema soka ndio ajira yake hivyo ana kila sababu ya kucheza kwa kujituma ili kuendesha familia yake na anatarajia changamoto mpya msimu ujao na uwezo wake haumpi presha. Hata hivyo, kuna taarifa kiungo huyo huenda katua Singida Big Stars (SBS).

SOMA NA HII  SIMBA YAPATA DAWA MPYA....OKRAH NDANI...IHEFU WAPANIA KUPIGA KWENYE MSHONO...