Home Habari za michezo BAADA YA KUONA YANGA KAMA WAMEMSUSA HIVI….YACOUBA ACHUKUA UAMUZI HUU…ADAI ANAPITIA KIPINDI...

BAADA YA KUONA YANGA KAMA WAMEMSUSA HIVI….YACOUBA ACHUKUA UAMUZI HUU…ADAI ANAPITIA KIPINDI KIGUMU…


Hatimaye Kiungo mshambuliaji wa Yanga Yacouba Songne amerejea kwao Burkinafaso kwa matibabu zaidi.

Yacouba ambae ameuguza majeraha kwa muda mrefu sasa baada ya kuumia mwanzoni mwa msimu uliopita bado ana mkataba na kalabu ya Yanga na alitajwa kutolewa kwa mkopo ili akapate nafasi ya kurudisha kiwango chake.

Yacouba alihusishwa na timu nyingi, huku Geita Gold ikionekana ndipo ambapo atakwenda staa huyo.

Lakini ghafla mambo yamebadilika na sasa Staa huyo amerejea kwa Burkinafaso.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagrama Yacouba ameandika;

“Msiwe na wasiwasi, kwa sasa napitia kwenye wakati mgumu lakini nitakuwa imara tena”

Yacouba amepewa program maalumu ambayo ataendelea kuitekeleza wakati wote akiwa nyumbani kwao Burkinafaso.

Yacouba hajaorodheshwa kwenye list ya majina ya Wachezaji wa Yanga msimu wa (2022/23) lakini ataendelea kuwa mchezaji wa Yanga.

SOMA NA HII  YANGA: HATUNA HOFU DHIDI YA SIMBA