Home Habari za michezo YANGA SC WAZIDI KUPANGA NA KUPANGUA SAFU ZA UTAWALA….BOSI KMC APEWA SHAVU...

YANGA SC WAZIDI KUPANGA NA KUPANGUA SAFU ZA UTAWALA….BOSI KMC APEWA SHAVU LA UMENEJA….


Klabu ya Yanga imeendelea kufanya mabadiliko ya uongozi baada ya Rais wa Klabu hiyo kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji, kumteua Saad Kawemba kuwa Mkurugenzi wa Mashindano, na kumteua Walter Harson kuwa Meneja mpya wa Kikosi hicho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu hiyo, Saad Kawemba anapewa majukumu hayo baada ya aliyekuwa kwenye nafasi hiyo, Thabith Kandoro kumaliza mkataba wake ndani ya Klabu hiyo.

Walter Harson ambaye alikuwa ni Katibu Mkuu wa KMC FC anakuwa Meneja wa timu hiyo ya Wananchi, akichukua nafasi ya Hafidh Saleh ambaye amepangiwa majukumu mengine ya kuwa Mratibu wa Timu. Uteuzi huo unaanza rasmi Agosti 1, 2022.

Hata hivyo, Yanga SC itazindua rasmi Wiki ya Mwananchi mapema, Agosti 1, 2022, kuelekea Siku ya Mwananchi, tayari Yanga SC wameunda Kamati yenye Wajumbe Saba wakiongozwa na Mwenyekiti Arafat Haji ambaye ni Makamu wa Rais wa Klabu hiyo.

Wajumbe hao ni Wakili Simon Patrick, CPA. Haji Mfikirwa, Taji Liundi, QS. Said Yassin Mrisho, Khamis Abeid Dacota na Christinah Oscar Korosso. Kilele cha Wiki ya Mwananchi kinatarajiwa kuwa Jumamosi ya Agosti 6, 2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

SOMA NA HII  KUHUSU HATMA YA LWANGA...AHMED ALLY AANIKA MPANGO WA SIMBA..ADAI WALITAKA KUMTEMA...