Home Habari za michezo WAKATI SIMBA WAKITAMBA KWA UBORA…YANGA WAIFUNIKA KWA JEZI BORA AFRIKA NZIMA…

WAKATI SIMBA WAKITAMBA KWA UBORA…YANGA WAIFUNIKA KWA JEZI BORA AFRIKA NZIMA…

Jezi ya nyumbani ya @yangasc imetajwa kama moja kati ya jezi bora za vilabu vya mpira barani Afrika ikiwa inashika nafasi pili nyuma ya jezi ya Zamalek SC @zscofficial ya nchini Misri.

Jezi hiyo ya Yanga imetajwa kama moja ya jezi zilizotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu pamoja na ubunifu wa kipekee ambao ulifanywa na @sheriangowi .

Jezi ya Simba ‘third kit’ nayo haijabaki nyuma kwani imetajwa kama jezi namba 9 kwa ubora barani Afrika.

Taarifa hizi zimetolewa na ukurasa maarufu wa michezo barani Afrika unaojulikana kama @africasoccerzone .

Je, ni ipi jezi bora zaidi kwako katika hizo 10 zilizoorodheshwa na mtandao huo? tuandikie kwenye comments hapo chini.

SOMA NA HII  KISA SIMBA 'KUFELI' MSIMU HUU....CHAMA AMTUPIA LAWAMA KOCHA MRAZILI...ADAI YEYE NDIO CHANZO..