Home Habari za michezo KIULAAINI KABISA…FEI TOTO AKUBALI YAISHE NA YANGA…ISHU YAKE YAACHWA KWA NABI….

KIULAAINI KABISA…FEI TOTO AKUBALI YAISHE NA YANGA…ISHU YAKE YAACHWA KWA NABI….

Habari za Yanga

Sakata la Yanga na kiungo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ liko hatua za mwisho kufikia tamati baada ya jana klabu hiyo kumrudisha jijini Dar es Salaam nyota huyo mzawa kwa mazungumzo ya mwisho ya kumrudisha kundini.

Hata hivyo inaelezwa suala la nyota huyo kuwepo uwanjani Jumapili Yanga itakapocheza na mchezo wa pili wa makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika limeachwa kwa kocha Nasreddine Nabi.

Za ndani kabisa zinaeleza kwamba, kiungo huyo fundi na Yanga walikuwa na mazungumzo na baada ya vikao vya kisiwani Zanzibar jana alitakiwa kuvuka maji kwa safari maalum ya kuja kuonana na tajiri wa Yanga, Ghalib Said Mohamed na rais wa klabu, Injinia Hersi Said ambaye amerejea jana nchini kutoka Makka, Saudi Arabia akikokuwa kwenye ibada ya Hija.

Ukiachana na suala la kumaliza tofauti za pande hizo mbili, jingine ni kuangalia uwezekano wa kumpa mkataba mnono mchezaji huyo ambaye kama atakubali dili hilo anaweza kuwa staa wa Kitanzania tajiri zaidi baada ya Yanga kufikiria kumpa mshahara wa sh 16.5 milioni kwa mwezi, huku dau lake la usajili ukijumlisha na gari linaweza kukaribia sh 400 milioni.

Kiungo huyo alipoulizwa kuhusu mkakati huo wa kumaliza tofauti na klabu yake, alishindwa kukubali au kukataa na kuishia kucheka akiomba kwanza afike jijini Dar es Salaam.

Makamu wa rais wa Yanga, Arafat Haji aliliambia gazeti hili kwamba haitakuwa jambo jipya kumuona Fei Toto uwanjani Jumapili kwa kuwa huyo ni kiungo wao na ni mali yao.

Arafat aliongeza na kukiri kuwa walikuwa katika mazungumzo ya kina na familia na hata mchezaji mwenyewe juu ya mustakabali wake huku akisema Yanga haishindwi kitu.

“Ukiniuliza kuhusu Feisal jibu langu litakuwa moja tu huyu ni mchezaji wetu, na kuhusu kucheza au kuwepo Jumapili ni suala la uamuzi wetu na makocha kwa kuwa huyu ni mwanafamilia na sherehe yetu ya Jumapili inamuhusu,” alisema Arafat.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA MKUDE NA NA KYOMBO KWENDA KUKIPIGA ULAYA...UKWELI WOTE HUU HAPA...