Home Habari za michezo KWA MAN UTD MPYA MBONA MTAKOMA AISEE…WAARABU WAPANIA KUMNUNUA MBAPPE….

KWA MAN UTD MPYA MBONA MTAKOMA AISEE…WAARABU WAPANIA KUMNUNUA MBAPPE….

Man UTD

MMESIKIA? Wakati kila bosi akipambana kwa ajili ya kuinunua Manchester United, hivi karibuni Mwenyekiti wa Benki ya Qatar Islamic, Sheikh Jassim bin Hamad Al Thani, alitangaza kuweka dau kwa ajili ya kuinunua timu hiyo, huku akielezwa anataka kumleta Kylian Mbappe kutoka PSG.

Al Thani ameweka dau hilo na kukubali kuingia kwenye vita dhidi ya mabilionea wengine ikiwa pamoja na Sir Jim Ratcliffe na Hedge Fund Elliott Investment Management.

Hata hivyo, mashabiki wengi wa Manchester United wanaonekana kuwa na imani sana na Al Thani kuliko mabosi wengine wanaoihitaji timu hiyo kutokan na mambo ambayo mwarabu huyo amedaiwa kuahidi atayafanya ikiwa atapewa haki ya kuimiliki timu hiyo.

Moja kati ya maeneo ambayo amepanga kufanya kufuru ni kwenye usajili wa dirisha la majira ya kiangazi ambapo kuna uwezekano akamshusha staa wa PSG, Kylian Mbappe.

Kiasi cha pesa ambacho wanataka kukitumia kwenye usajili wa dirisha lijalo kinaweza kuwa mara mbili zaidi ya kile cha Pauni 200 milioni ambacho familia ya Glazer ambayo ndio mmiliki wa sasa wa timu hiyo ilikitumia katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana.

Taarifa kutoka tovuti ya ESPN, zimefichua kuwa mpango wa Sheikh Jassim ni kutumia gharama yoyote ili kuweza kuirudisha timu hiyo kwenye zama zake za zamani na moja ya maeneo aliyipanga kuyaweka sawa ni usajili wa kishindo.

“Mpango uliowasilishwa umejumuisha mchakato wa kuirudisha timu kwenye zama zake kuanzia ndani na nje ya uwanja na zaidi kuwafanya mashabiki wawe karibu na timu, tutawekeza kwenye timu zote kuanzia za vijana hadi wanawake, kutanua uwanja na kuboresha miundombinu,”Ilisema taarifa ya waarabu hao mara baada ya kuweka ofa.

Taarifa kutoka ESPN zimeeleza kwamba kuna uwezekano wa Mbappe kutua kutokana na uhusiano wa karibu uliopo baina ya Jasmin Al Thani na mwenyekiti wa PSG Nasser Al-Khelaifi ambao wote wanatokea Qatar na Al-Khelaifi ndio ametajwa kuwa mtu anayemuongoza na kumshauri tajiri huyo ili kukamilisha mchakato wake wa kuichukua timu hiyo.

Katika kipindi cha hivi karibuni Kylian Mbappe amekuwa akidaiwa kutaka kuondoka na badala ya kumuuza kwa timu nyingine ukaribu kati ya vigogo hao wawili unatoa uhakika wa zaidi ya asilimia 70 kwamba fundi huyo atatua kwenye viunga vya Man United ikiwa ataondoka PSG.

Vilevile mpango wa Al Thani ni kuifanya Man United iwe na mchezaji staa wa Dunia kama ilivyokuwa kwa Manchester City na Erling Haaland, kwa sasa staa pekee anayeonekana kuwa habari ya mjini ni Mbappe.

Mbali ya pesa za waarabu hao Man United pia itakuwa na uhuru mkubwa wa kununua mastaa wapya na kuepukana na tungu la sheria za matumizi ya pesa kwa sababu haijafanya usajili wa pesa nyingi katika dirisha la majira ya baridi ikiwa imewasajili Marcel Sabitzer, Wout Weghorst na Jack Butland ambao wote wametua kwa mkopo wa nusu msimu.

Vilevile kwenye dirisha lijalo wamepanga kuwauza baadhi ya mastaa ambao wameshindwa kumshawishi kocha Erik Ten Hag na mmoja kati yao ni kapteni wao Harry Maguire na pesa watakazozipata wanaweza kuzitumia pia kwenye kuvuta mastaa wapya ikiwa pamoja na huyo Mbappe.

“Kwa muda mrefu, nafikiri Ligi Kuu England ilikuwa ni mbio za farasi wawili, lakini kwa sasa tupo sita, saba hadi nane nafikiri ushindani umeongzwa na mipango na pesa, nipo hapa kwa ajili ya kufundisha timu na kuifanya iwe bora lakini bado nahitaji wachezaji bora ili kufanya vizuri zaidi na ili kuwapata lazima nifanye mahojiano na mabosi”alisema Ten Hag mapema mwezi huu juu ya uwezekano wa kusajiliwa wachezaji wakubwa ikiwa pamoja na Kylian Mbappe.

SOMA NA HII  MIAKA 89 YA YANGA ILIVYOSHEREKEWA KIBABE MBEYA LEO HII...MZIZE, PACOME NI BALAAH...