Home Uncategorized YANGA WATUPA JIWE GIZANI, WATAMBA KUWA WANAANZA NA KUKU KISHA VIFARANGA VITAFUATA

YANGA WATUPA JIWE GIZANI, WATAMBA KUWA WANAANZA NA KUKU KISHA VIFARANGA VITAFUATA



BAADA ya picha ya aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa kuonekana akiwa na watu wa Yanga ikiwa ni pamoja na Injinia, Hersi Said inaelezwa kuwa tayari wameshaanza kufanya masuala yake taratibu kuingia mtaa wa pili.

Habari kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa wameanza kazi taratibu kujibu mapigo ndani ya mtaa wa pili hivyo mengine yanakuja:- “Ni kweli kuna picha ambayo imeonekana na alikuwa ni Senzo lakini siwezi kuzungumzia alikuwa anafanya nini.

“Ukitaka kuchukua vifaranga anza na mama kwanza kisha wengine watafuata ndivyo ilivyo hivyo tumeanza na mama kisha vifaranga vitafuata.

“Tumekuwa na utaratibu wa kuchukua wachezaji wetu kutoka kwetu na wao pia wamekuwa wakichukua wachezaji kwetu, walimchukua Niyonzima, Gadiel ila hatujasema kitu nasi pia tulikuwa tunachukua wachezaji wao.

“Lakini kuna watu ambao wamekuwa na ukorofi na wanavuruga mpira, sisi tuliokuwa tumekaa mafichoni sasa tumeamka ili tuonyeshane nani atalia ama atacheka,” ilieleza taarifa hiyo.

SOMA NA HII  SIMBA YATAJA KILICHOWAPONZA KUNYOOSHWA BAO 1-0 NA YANGA