Home Habari za michezo KUHUSU MZIZA NA NAMNA ANAVYOCHEZA YANGA…NABI KATIKISA KICHWA WEE..KISHA AKASEMA HAYA…

KUHUSU MZIZA NA NAMNA ANAVYOCHEZA YANGA…NABI KATIKISA KICHWA WEE..KISHA AKASEMA HAYA…

Habari za Yanga SC

Kiwango anachokionyesha straika wa Yanga, mzawa Clement mziza kwa dakika anazopewa na kocha Nasreddine Nabi, zinamuweka kwenye wakati mgumu Chrispin Ngushi kupata nafasi ya kucheza.

Kocha Nabi amekuwa akimpa dakika chache Mziza ambaye amepandishwa kutoka kikosi B na anazitumia vizuri hadi sasa alifunga mabao ya kuipa Yanga pointi.

Katika mabao matatu aliyofunga Ligi Kuu Bara, Mziza aliisaidia kuipa Yanga pointi sita baada ya kufunga dhidi ya Kagera Sugar ilikuwa 1-0 na KMC timu yake ikishinda 1-0 pia alifunga mojawapo kati ya mabao 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania.

Jambo ambalo kocha Nabi alisema bado ni kijana mdogo ndio maana wanampa dakika chache ili kumjengea kujiamini kufanya makubwa zaidi kwenye karia yake, akiamini kuna kitu anakiongeza kila anapocheza.

“Kadri ninavyompa dakika za kucheza ndivyo kiwango chake kinazidi kukua siku hadi siku, kikubwa akijengeka kujiamini atafanya mambo makubwa zaidi kwani soka linahitaji ushindani, nidhamu na kujituma kwa bidii;

Aliongeza “Pia maarifa yake ya kazi yatazidi kuongezeaka maana atajifunza mbele ya wengine ili kuboresha kiwango chake.”

Ukiachana na mabao ya Ligi Kuu, Mziza anamiliki mabao sita kwenye Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), tofauti na ngushi ambaye kwa msimu huu hana bao hata moja, hivyo atahitaji kupambana zaidi ili kumshawishi kocha kumpa dakika za kucheza.

Baada ya Mziza kuonyesha kiwango ligi ya ndani, juzi kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Bamako ya Mali, Nabi alimpa dakika 14.

Dakika ya 76 Nabi alifanya mabadiliko kwenye mchezo huo alimtoa Kennedy Musonda, akaingia Mziza ambaye aliongeza presha kwa mabeki wa Bamako.

Hilo pia Nabi alilizungumzia kwamba “Muda niliompa ni sahihi, kuna kitu atakuwa amekipa kwenye michuano hiyo inayohitaji kutumia nafasi kwa umakini zaidi.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUISHIA JUKWAANI MSIMU ULIOPITA...MAKAMBO AVUNJA UKIMYA KUHUSU YANGA MPYA...ATOA MSIMAMO WAKE...