Home Habari za michezo KISA MECHI YA SIMBA vs VIPERS…AHMED ALLY ‘AWANYEA’ WACHAMBUZI BONGO…”SEMENI MPAKA NUSU...

KISA MECHI YA SIMBA vs VIPERS…AHMED ALLY ‘AWANYEA’ WACHAMBUZI BONGO…”SEMENI MPAKA NUSU FAINAL”…

Habari za Simba SC

Baada ya Simba kufanikiwa kuibuka na alama tatu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa hatua ya Makundi wakiichapa Vipers FC bao 1-0.

Wachambuzi wengi wa soka nchini wameonekana kutofurahishwa na kiwango cha Simba kinachooneshwa  katika michezo yake msimu huu huku wengi wakisema sio timu wanayoifahamu.

Sasa Meneja wa Habari na Mawasiliano , Ahmed Ally kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe ambao unaonekana kuwalenga wachambuzi.

Ahmed ameandika;

“Ukisikiliza Radio unaweza kujua Simba ndo imefungwa , halafu ukisiliza tena unaweza kudhani  ndo ina point moja kwenye kundi letu, halafu ukitega sikio vizuri unaweza kuhisi kwamba  hakuna kitu kizuri tumefanya jana

Ila sisi ndo tunapenda mtukosoe hadi tufike Nusu Fainali tuliyokusudia”.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA...RUVU SHOOTING 'WAJICHUA' KWA MASAA MANNE JUANI..