Home Habari za Yanga NABI ATANGAZA HALI YA HATARI…SILAHA ZA KUTISHA ZAIDI ZANOLEWA…ISHU NZIMA IKO HIVI

NABI ATANGAZA HALI YA HATARI…SILAHA ZA KUTISHA ZAIDI ZANOLEWA…ISHU NZIMA IKO HIVI

NABI ATANGAZA HALI YA HATARI...SILAHA HATARI ZAIDI ZANOLEWA...ISHU NZIMA IKO HIVI

Jeshi la Kocha Mkuu wa Yanga Mtunisia, Nasreddine Nabi juzi liliingia kambini tayari kwa mchezo wa mwisho wa makundi wa Kombe la Shirkisho Afrika huku likianza na program ya fiziki pekee.

Yanga katika mchezo huo, watacheza dhidi ya TP Mazembe Aprili 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa TP Mazembe, Lubumbashi nchini DR Congo saa 10:00 Jioni.

Katika mchezo huo, Yanga wataingia uwanjani kwa ajili ya
kukamilisha ratiba pekee, kwani tayari wameshafuzu katika Kundi, D huku TP Mazembe wakitaka kulipa kisasi cha kufungwa mabao 3-1.

Akizungumza nasi, Nabi alisema kuwa mchezo huo wanauchukulia umuhimu mkubwa, kwani wanazihitaji pointi za TP Mazembe ili wabakie kileleni katika msimamo ambao wana pointi 10 sawa na US Monastir waliofuzu hatua ya robo fainali.

Nabi alisema kuwa, kikosi chao kimeingia kambini juzi Jumatatu kikiwa chini ya kocha msaidizi Mrundi Cedric Kaze kwa kuanzana program ya fitinesi pekee kukimbia mbio fupi na ndefu kwa ajili ya kurejesha utimamu wa mwili wachezaji wao.

SOMA NA HII  RIVERS UNITED WAZIDIWA KETE NA YANGA...WACHACHAWA! WAPAGAWA!...ISHU NZIMA IKO HIVI