Home Habari za Yanga FARID MUSSA ATOBOA SIRI GOLI ALILOWAPIGA MAZEMBE…AMEZUNGUMZA HAYA

FARID MUSSA ATOBOA SIRI GOLI ALILOWAPIGA MAZEMBE…AMEZUNGUMZA HAYA

YANGA YAWEKA REKODI HII MPYA...HAKUNA TIMU ILIYOWAHI...AFRIKA YATETEMA

FARID Mussa ndiye alikuwa shujaa akitokea benchi na kuifungia bao la ushindi Yanga dhidi ya TP Mazembe huku akisema ukuta wa wapinzani wao ulikuwa mgumu.

Farid alifunga bao hilo na Yanga kufikisha pointi 13 kwenye kundi D ikifuatiwa na US Monastir nao wakiwa na pointi hizo lakini inashika nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao.

Farid alisema; “Nilipokuwa benchi kocha alinisisitiza kuwasoma mabeki wao huku akinisisitiza pia kuwa kwa asilimia kubwa ni wachezaji ambao hawakuwaona mchezo wa kwanza hivyo baada ya kupata nafasi na wao waliingia kuonyesha walichonacho ndio ugumu tuliokutana nao”

“Bao nililofunga lilikuwa linahitaji maamuzi ya haraka kama nilivyofanya kwani ulikuwa ni mpira wa kutemwa na sio makosa ya mabeki nilipoipata hiyo nafasi sikutaka kufanya mambo mengi nilijiweka sawa na kukwamisha mpira nyavuni na nashukuru ndilo lilikuwa bao la ushindi,” alisema.

Farid alisema anafurahi kuwa mmoja wa wachezaji ambao wameifikisha timu kwenye malengo waliyojipangia baada ya kutinga hatua ya makundi kuhakikisha wanafanya vyema na kucheza hatua ya robo.

Alisema baada ya kutinga hatua hiyo, wao kama wachezaji malengo ni kuona wanacheza fainali ya mashindano hayo huku akiweka wazi kuwa hilo linawezekana kutokana na ubora wa kikosi chao na chachu ya mafanikio waliyonayo wao kama wachezaji.

Mbali na Yanga timu nyingine zilizofuzu hatua ya robofainali kwenye Shirikisho ni Asec Memosas, AS FAR, Marumo, Rivers United, USM Algiers na Pyramids. Kati ya hizo Yanga inaweza kupangwa na Pyramids (Misri), Rivers United(Nigeeria ) au USM ya Algeria.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSHUHUDIA 'AKIBABULIWA CHA UCHUNGU'...PABLO ASALIMU AMRI KWA NABI...ADAI WALIZIDIWA KILA KONA...