Home Habari za michezo HIKI HAPA KILICHOWAPONZA SIMBA…MECHI DHIDI YA RAJA CASABLANCA

HIKI HAPA KILICHOWAPONZA SIMBA…MECHI DHIDI YA RAJA CASABLANCA

Habari za Simba

Mchezo wa juzi Jumamosi, dhidi ya Raja Casablanca, Simba kuna kitu walijaribu kukionyesha lakini changamoto kwao ni makosa yaliyofanyika kwenye safu ya ulinzi.

Pindi unapokutana na timu kubwa kama Raja Casablanca yenye wachezaji wakubwa kama wakina Amza Khaba lazima watatumia makosa yakoo kwa ufasaha watafunga mabao.

Simba SC wanaelekea hatua ya robo fainali hatua ambayo unakutana na timu nyinga zenye uwezo kama Raja ama zaidi ukifanya makosa kama yale utakuwa unajiweka kwenye wakati mgumu.

Mwalimu Robertinho anatakiwa kuja na mpango wa muda mfupi kuiandaa timu yake kwenye michezo mikubwa inayofwata ajaribu kuangalia namna ambavyo safu ya ulinzi inaweza kupunguza makosa.

Pia anatakiwa kuwa na mpango wa muda mrefu kwa maana ya kuanza kufwatilia mchezaji mwenye uwezo mkubwa na ataongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi.

SOMA NA HII  FUNDI MPYA WA YANGA NI BALAA NA NUSU....KAZI YAKE YA KWANZA HII HAPA...