Home Habari za michezo MUSONDA ALALAMIKA RATIBA KUWA NGUMU…ANA UCHU ILE MBAYA…AMEZUNGUMZA HAYA

MUSONDA ALALAMIKA RATIBA KUWA NGUMU…ANA UCHU ILE MBAYA…AMEZUNGUMZA HAYA

Habari za Yanga

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Kenedy Musonda amesisitiza kwamba kuna moto unakuja kimataifa. Amesema walishafanya mengi ndani ya Tanzania sasa wanataka kutisha kimataifa haswa robo na nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.

Musonda aliyejiunga na Yanga dirisha dogo la usajili alisema wao kama wachezaji wapo tayari.

“Nimecheza mechi nyingi za mashindano ya ndani na kimataifa nje ya Yanga lakini tangu nimetua hapa nimegundua utofauti mkubwa ni nchi ambayo mashabiki wanapenda sana mpira wapo na timu zao nyakati zote;

“Wachezaji wa timu wanatambua hilo wamekuwa wakipambana kuwapa furaha pia Yanga ina timu bora ambayo naiona ikifanya vizuri zaidi kimataifa baada ya kuonyesha ubora kwenye ligi ya ndani ambayo tunapambana kutetea taji na hilo lipo wazi kuwa linawezekana.

Musonda alisema wao kama wachezaji baada ya kupambana na kufanikiwa kuongoza kundi sasa wanataka kuionyesha Afrika walichonacho. Alisema kila mchezo ulio mbele yao wanauchukulia kwa ukubwa kwasababu wapo kwenye hatua nzuri ya kutetea ubingwa wa ligi, wana nafasi nzuri ya kufanya vizuri FA na kufika hatua nzuri kwenye mashindano ya kimataifa kutokana na ubora wa kikosi walichonacho.

“Tuna timu nzuri wachezaji ni wapambanaji na wana uchu wa mafanikio ukimuangalia mchezaji mmoja mmoja unaona anapambana kutafuta nafasi ili kuonyesha kile alichonacho na benchi la ufundi limekuwa likitoa nafasi.” alisema. Akizungumzia mechi za ligi na FA alisema wana ratiba ngumu na mechi ngumu lakini hilo haliwaondoi kwenye mstari watafanya kila kitu kuhakikisha wanapata matokeo na kusonga mbele.

“Kocha katuambia michezo yote ina umuhimu tunatakiwa kupambana kuhakikisha tunapata matokeo Aprili kuna mechi tatu Geita Gold, Singida Big Stars na Simba sijapata bahati ya kukutana na timu mbili kati ya hizo sitaweza kuzungumza sana lakini mchezo wetu wa FA tunacheza na timu ambayo tayari nimeshaifunga.” Kwenye droo ya jana usiku Yanga imepangwa na Rivers United ya Nigeria.

SOMA NA HII  GAMONDI AFICHUA MBINU ZA KUIMALIZA AZAM FC... SIENDI KWA KULIPA KISASI