Home Habari za michezo BAADA YA KUTEMWA JANA….AKPAN NAYE KAONA ISIWE TABU….ONA ALIYOYASEMA KWA MABOSI WA...

BAADA YA KUTEMWA JANA….AKPAN NAYE KAONA ISIWE TABU….ONA ALIYOYASEMA KWA MABOSI WA SIMBA…

Habari za Simba

Uongozi wa Simba ilitangaza kuachana na kiungo Mnigeria Victor Akpan ambaye alijiunga na timu hiyo Julai 2022 kutoka Coastal Union,kwa mkataba wa miaka miwili.

Akpan ametumikia mkataba wake kwa mwaka mmoja akitumia nusu msimu Simba na nusu Ihefu alipoenda kwa mkopo.

Akpan kupitia akaunti yake ya Instagram amewashukuru viongozi na mashabiki wa Simba na Klabu imemfanya kuwa imara na jasiri

“Napenda kutumia fursa hii kuwashukuru mashabiki wote wa klabu ya Simba na Uongozi wote kwa nafasi nzuri ya kuwa sehemu ya familia kubwa katika kipindi changu kwenye klabu, kwa kweli haikuisha kama nilivyotarajia lakini kuna mengi nimejifunza”.

“kucheza katika klabu hii kumenifanya niwe imara na mwenye kujituma zaidi, jasiri na nimebaki na kumbukumbu ,nzuri moyoni mwangu”.

“Kama inavyosemwa kila chenye mwanzo pia kina mwisho wa awamu nyingine, Mungu awabariki wote”

Kiungo huyo alisajiliwa kwenye dirisha kubwa la usajili msimu huu na alitolewa kwa mkopo kwenda Ihefu kwenye dirisha dogo la usajili msimu 2022/23..

Tayari Simba imeachana na wachezaji wawili wa kigeni ambao ni Akpan na Augustine Okrah.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTWAA NGAO YA JAMII, SIMBA WASEMA HAYA KUHUSU MAKOMBE YALIYOBAKIA