Tetesi za Usajili Yanga
Habari za michezo

BAADA YA SIMBA KUMTEMA MKUDE KOCHA WA YANGA KUAMUA JAMBO HILI

Staff Desk July 12, 2023 12:08 pm

Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans wameshamalizana kimazungumzo na Kiungo Mzawa, Jonas Mkude lakini imeliacha faili lake kwa Kocha Miguel Gamondi afanye uamuzi wa mwisho muda wowote juma hili atatangazwa.

Mkude aliitumikia Simba SC kwa zaidi ya miaka 10 kwa mafanikio, lakini klabu hiyo ya Msimbazi ilimtema ikiwa ni sehemu ya kujipanga upya baada ya kupoteza makombe kwa msimu miwili mfululizo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Young Africans zinadai baada ya majadiliano ya muda mrefu baina ya Mkude na klabu hiyo, na sasa inasubiriwa kauli ya Gamondi ili Mkude asaini na kutangazwa.

Uwezekano wa Mkude kusainishwa ni mkubwa kutokana na uzoefu wake ambao hata Gamondi ameelezwa lakini hata gharama yake ni ndogo kwani yuko huru na amekubaliana na masharti ya Young Africans.

Young Africansa itampa Mkataba wa mwaka mmoja wenye masharti ya kumuongeza kama kiwango kitamridhisha Kocha Miguel Gamondi.

Usajili wa Mkude unaenda kuongeza ushindani kwenye kiungo alipo Khalid Aucho na Yanick Bangala na mastaa wengine.

YANGA WASHINDWA KUMZUIA MAYELE, ATIMKIA TIMU HII USAJILI WAKE KUFURU KOCHA WA YANGA AKUTANA NA MASTAA WA KLABU HIYO LEO KWA MARA YA KWANZA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply