KLABU ya Yanga imetangaza kumuuza mchezaji wake Yannick Bangala katika timu ya Azam.
Bangala hakuwemo kwenye utambulisho wa wachezaji katika kilelele cha Wiki ya Mwananchi Julai 22, 2023 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
“Uongozi wa Young Africans SC unapenda kuutarifu Umma kuwa tumefikia makubaliano na Klabu ya Azam FC kumnunua mchezaji wetu Yannick Bangala,” imesema Yanga kupitia mitandao yake ya kijamii.




