Home Habari za michezo BAADA YA VUGUVUGU LA KUACHWA WACHEZAJI WENGI… WAKALA WA JEAN BALEKE AFUNGUKA...

BAADA YA VUGUVUGU LA KUACHWA WACHEZAJI WENGI… WAKALA WA JEAN BALEKE AFUNGUKA HATMA YA BALEKE SIMBA

Habari za Simba

Mukandila ni mmiliki wa Kampuni ya uwakala ya Bro Soccer Management inayowasimamia wachezaji 20 na Kocha mmoja.

Yeye na Martin Lubula ndio wako nyuma ya Clatous Chama,Jean Baleke, Yannick Bangala, Djuma Shabani,Gibril Sillah,Mundele Makusu na wengine wengi.

Kwenye orodha ya wachezaji wanaosimamiwa na Faustino Mukandila mchezaji mwenye thamani kubwa ni Mshambuliaji wa Qatar Sc Ben Malango mwenye thamani ya €1.50m akifuatiwa na Arsene Zola €800k etc

Mukandila pia anamsimamia Fabrice Luamba Ngoma mwenye thamani ya €400k.

Kwa mujibu wa Martin Lubula ambaye ni Business Development wa Bro Soccer Management anasema Fabrice Ngoma ameshapata timu nyingine tayari na muda wowote watatoa taarifa ya wapi anakwenda huku akisema Baleke ataendelea kusalia Simba mpaka mwisho wa msimu ujao.

SOMA NA HII  SIMBA WAELEKEZA NGUVU ZAO LIGI KUU