Home Habari za michezo KOCHA WA YANGA GAMONDI ANENA NA MASHABIKI, ASEMA HAYA

KOCHA WA YANGA GAMONDI ANENA NA MASHABIKI, ASEMA HAYA

Kocha Mpya wa Yanga

KOCHA Mkuu wa klabu ya Yanga Miguel Gamondi amesema hana shinikizo lolote kuelekea msimu ujao na anaimani yakufanya vizuri akiwa na mabingwa hao wa soka la Tanzania.

Miguel amezungumza na Dailynews Digital Julai 19, 2023 ambapo amesema yupo tayari kuianza safari yake huko Jangwani.

Kocha huyo raia wa Argentina amesema kwa muda mchache aliokaa na kikosi chake amewaona wachezaji wanaojituma na kujitambua kitu ambacho kinampa imani ya kufanya vizuri na timu hiyo na hana wasiwasi wowote.

” Nimezoea kufanya kazi katika shinikizo hasa katika soka la Afrika, mashabiki wanahitaji matokeo muda wote kwa hiyo ni lazima ukiwa kocha ujue kuishi katika nyakati zote ukiwa umeshinda au umepoteza”amesema Gamondi

Alipoulizwa kuhusu kivuli cha benchi la ufundi lililopita ndani ya timu hiyo kocha Miguel amesema anaheshimu kile kilichofanywa na watangulizi wake na anatamani kufanya zaidi ya walipoishia ndio maana ameanza mapema kukisuka kokosi hicho.

Kocha huyo ameongeza kwa kusema anavutiwa mno na mazingira ya Tanzania hasa tamaduni za mashabiki wa soka la bongo kujitokeza kwenye matukio mbalimbali yanayozihusu timu zao.

SOMA NA HII  MO DEWJI ATEUA MABOSI WAPYA 21 SIMBA....KADUGUDA, MZEE DALALI NAO WAULA...