Home Habari za michezo MAJANGA RUVU SHOOTING MBIONI KUPIGWA MNADA…. MASAU BWIRE AFUNGUKA KILA KITU

MAJANGA RUVU SHOOTING MBIONI KUPIGWA MNADA…. MASAU BWIRE AFUNGUKA KILA KITU

Klabu ya Ruvu Shooting imeshuka daraja kutoka Ligi Kuu Bara na msimu ujao itacheza Ligi ya Championship, huku ikidaiwa timu hiyo ipo kwenye mpango wa kupigwa bei.

Ruvu ilikuwa timu ya kwanza kushuka daraja msimu uliopita kwa kuburuza mkia pamoja na Polisi Tanzania na Mbeya City, baada ya kupanda msimu wa 2017-2018 inadaiwa mabosi wake wanasubiri mtu wa kuinunua ili kuachana nayo jumla.

Habari zinaeleza kuwa mabosi wa timu hiyo wanataka kuwekeza nguvu zaidi kwenye timu moja ya JKT Tanzania, hivyo wanatafuta mtu atakayeweza kuinunua Ruvu.

Chanzo hicho kimesema; “Kuna mpango huo ingawa sidhani kama jambo hili litafanikiwa, kununua timu sio kazi kubwa, kazi ipo kwenye uendeshaji.”

Hata hivyo, viongozi wa Ruvu hawajatangaza mchakato wowote wa kuuzwa kwa timu na hata msemaji wa klabu hiyo, Masau Bwire alipotafutwa kuulizwa juu ya mchkato huo alisema kama upo watautangaza rasmi.

“Kwani mmesikia wapi? Kukiwa na mpango huo tutatangaza rasmi,” amesema Masau kwa kifupi.

SOMA NA HII  CHANONGO AWAONYA MASTAA WENZIE KWENYE ISHU HII