Home Habari za michezo SAKHO ASEMA HAYA KWA MARA YA KWANZA TANGUA AONDOKE SIMBA

SAKHO ASEMA HAYA KWA MARA YA KWANZA TANGUA AONDOKE SIMBA

Siku moja baada ya kuthibitika ameondoka Simba SC na kujiunga na Klabu ya Quevilly Rouen Metropole (QRM) ya nchini Ufaransa, Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Senegal Pape Ousmane Sakho, ametoa neno la shukurani kwa Wanasimba SC.

Sakho aliyesajiliwa Simba SC msimu wa 2021/22 akitokea Teungueth FC ya nchini kwao Senegal, ametoa neno hilo la shukurani kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kiungo huyo ameonesha alikuwa na mazingira mazuri ya kimaisha klabuni hapo, kutokana na ushirikiano mkubwa alioupata kutoka kwa Viongozi, Wachezaji wenzake, Mashabiki na Wanachama.

Sakho ameandika: Ni vigumu sana kusema kwaheri. Ulikuwa uamuzi mgumu kufanya, lakini soka ndivyo lilihivyo. Jambo muhimu zaidi kwangu ni kwamba sisi tayari ni familia, na mmeniunga mkono kila wakati. Sina hata maneno ya kuelezea jinsi nilivyo na huzuni. Nadhani soka ni kujaribu kupanda viwango, lakini fahamu kuwa @simbasctanzania bado ni familia yangu.

Wanasimba, ninawaona kila mahali, na ninataka kusema asante kwa upendo wenu. Naipenda Simba, na itakuwa hivyo daima. Ipo siku nitawaeleza wanangu maana ya Simba. Asante sana, na ninatamani timu ishinde kila kitu. Shukrani kwa wachezaji wote, viongozi wa Simba, Kocha na Wafanyakazi wote. Vikombe vyote, InshaAllah. Shukrani kwa klabu yangu mpya @qrm_2015 kwa kunipa nafasi ya kwenda kiwango cha juu zaidi. Kwaheri, familia

SOMA NA HII  MANARA ATUA MAKKAH, AWAOMBA WATANZANIA JAMBO HILI

1 COMMENT