Home Habari za michezo SIMBA BAADA YA KUMPA THANK YOU SAWADOGO, MAPYA YAIBUKA

SIMBA BAADA YA KUMPA THANK YOU SAWADOGO, MAPYA YAIBUKA

Habari za Simba

SIKU chache tu tangu apewe ‘Thank You’ na klabu ya Simba baada ya kukubaliana kuvunjiwa mkataba wa kuichezea timu hiyo, kiungo mkabaji Ismael Sawadogo ameibua mapya.

Sawadogo alisajiliwa na Simba katika dirisha dogo la usajili akitokea Difaa El Jadida ya Morocco kwa mkataba wa miaka miwili ametumikia miezi sita tu na kupewa mkono wa kwaheri kutokana na kushindwa kuendana na kasi ya timu hiyo baada ya mjaala mrefu kabla ya kuvunjwa kwa mkataba.

Mara baada ya msimu kumalizika mchezaji huyo aliingia makubaliano na Simba ya kuvunja mkataba ambapo kwa mujibu wake ameliambia Mwanaspoti kuwa amelipwa fedha ya mwaka mmoja kwaajili ya kuvunja mkataba na makubaliano ya kulipwa mshahara wa miezi sita iliyobaki.

“Bado nina mkataba wa miezi sita na Simba ambao tulikubaliana kulipana mshahara kila mwezi hadi nitakapomaliza hiyo miezi sita lakini imekuwa tofauti kwani wanakwenda kinyume na makubaliano,” alisema Sewadogo na kuongeza;

“Nawadai mshahara wangu wa mwezi wa sita hawajaniingizia na tayari nimeongea na Mwanasheria wa Simba, Hossea lakini jibu lake ni kwamba nitatumiwa kesho maongezi yalifanyika kabla hawajasafiri kwenda kwenye maandalizi ya msimu mpya.”
Sawadogo alisema hakuishia hapo akafanya juhudi za kumtafuta Mwenyekiti wa timu hiyo, Murtaza Manungu ambaye alimtumia ujumbe kwa meseji hadi jana hakupewa jibu lolote.

“Nimemtumia ujumbe Mwenyekiti pia hajaonyesha ushirikiano kwasababu sijajibiwa hivyo nimemjulisha mwanasheria wangu na kumuachia suala hilo alishughulikie,” alisema Sawadogo na kuongeza;

“Nimeomba kulipwa fedha za miezi mitatu na kuvunjiwa mkataba ili niweze kutafuta timu nyingine lakini hawataki kunipa ushirikiano na mshahara hawanilipi kama makubaliano yalivyokuwa.”

Uongozi wa Simba walitafutwa jana kufafanua jambo hilo ila simu zao ziliita bila majibu

SOMA NA HII  KISA KIPIGO CHA JANA...BENCHIKHA APONDA MASTAA SIMBA..."HATUNA WACHEZAJI HAPA..."