Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA NKANE…YANGA WATOA TAMKO HILI LEO…

KUHUSU ISHU YA NKANE…YANGA WATOA TAMKO HILI LEO…

Hali ya Mchezaji wa Yanga, Denis Nkane inaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu ya ziada hospitalini.

Nkane alianguka vibaya wakati akigombea mpira na beki wa Bullets na kupoteza fahamu kwa dakika kadhaa uwanjani kabla ya refa kuita gari la huduma ya kwanza na kumtoa uwanjani kwenye mechi iliyomalizika jioni hii jijini Lilongwe, Malawi ambapo Young Africans SC imetoka suluhu dhidi ya Nyasa Big Bullets kwenye mchezo wa Kimataifa kirafiki uliochezwa kwenye dimba la Bingu Mutharika kama sehemu ya kusherekea siku ya uhuru wa miaka 59 ya taifa la Malawi.

Baada ya matibabu kutoka kwa jopo la madaktari , Nkane alizinduka na kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

“Fahamu zake zimerejea kwa sasa, alipata mpasuko kidogo sehemu ya kichwa. Tumepanga tukifika Dar Es Salaam tumfanyie vipimo zaidi,” alisema Moses Etutu, Daktari wa Yanga.

Tunamtakia Afya Njema Denis Nkane.

SOMA NA HII  MASAUBWIRE ARUKA NA SIMBA, YANGA KISA HIKI HAPA