Achana na Skudu Makudubela, Max Nzengeli, Attohoula Yao, Clement Mzize, Ibrahim Bacca, Mudathir Yahaya wameupiga mwingi sana.
Yanga wana Timu ya kutetea mataji yao, Yanga wana wachezaji wanaotoa jasho lao kuipigania nembo ya Klabu dakika ya kwanza mpaka filimbi ya mwisho. Nadhani hapa ndipo ulipo utofauti wao na timu nyingine kwenye ligi yetu.
Kipindi cha kwanza viungo wa Azam walifanya kazi kubwa sana kuwakaba Yanga na walifanikiwa kwa hilo, kila eneo walifika lakini kipindi cha pili tayari walikuwa wameshakata moto kutokana na energy kubwa waliyoitumia kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Yanga walifanikiwa kuwafungua Azam kwa asilimia zaidi ya 90, walikosa utulivu tu wangefunga mabao mengi sana, mpaka mabao mawili ya Yanga yanafungwa utaona kabisa tayari Azam walikuwa wameshakubali na wametepeta.
Azam Fc licha ya kusajili vizuri, bado hawana ile hali ya pambanaji. Kukosekana kwa Amoah na makosa ya Zuberi Foba yaliwafanya washindwe kujiamini hasa kipindi cha pili na kuwaruhusu Yanga wapress langoni kwao huku Azam Fc wakishindwa kabisa kushambulia.
FT: Yanga 2-0 Azam Fc
⚽Aziz Ki
⚽Mzize
Pamoja na kiwango kibovu walichokionesha Azam Fc,bado wakikutana na Simba wanaweza kutawala mchezo na kushinda.
I am very happy to be with them sok la bongo