Home Habari za michezo MAJANGA HAFIZ KONKANI AGOMA KUVAA VIATU VYA MAYELE, ISHU IKO HIVI

MAJANGA HAFIZ KONKANI AGOMA KUVAA VIATU VYA MAYELE, ISHU IKO HIVI

hafiz konkani

Mshambuliaji mpya wa Klabu ya Yanga, Hafizi Konkoni amesema kuwa amekuja Yanga kuwatumikia Wananchi na si kuvaa viatu vya aliyekuwa mshabuliaji kwa timu hiyo Fiston kalala Mayele ambaye ametimkia Pyramids FC.

Konkoni amesema hayo wakati akihojiwa na Yanga TV, Kambini Avic Town na kuongeza kuwa yeye atafanya kazi yake kama Konkini na si kama mayele kwa sababu Mayele amefanya makubwa ndani ya klabu hiyo na yeye atafanya kwa uwezo wake kufikia malengo ya Klabu.

Konkini (23) amesajiliwa na Yanga hivi karibuni akitokea Bechem United FC ya Ghana ambayo ameitumikia kwa miaka saba.

“Nimefurahi sana kwa mapokezi, haikuwa rahisi kujiunga na moja ya klabu kubwa Barani Afrika. Mimekuwa nikiifuatilia Yanga kwa muda mrefu, hata hivi karibuni kwenye mashindano ya CAFCC nimefuatilia baadhi ya mechi, ni klabu bora na ninajisikia furaha kujiunga nah ii klabu.

“Straika aliyekuwa Yanga, Fiston Mayele amefanya makubwa, hivyo mashabiki wanategemea makubwa zaidi kutoka kwangu, nitajitahidi kuwa Hafizi Konkoni, siwezi kuwa Mayele, nitatoa mchango wangu wote kwa timu ili kuwapa furaha mashabiki.

“Yanga ina mashabiki wengi na wanapenda sana soka, wana vibe kubwa. Mayele amekuja hapa hakuwa na jina, lakini leo anafahamika Afrika nzima, kwa hiyo Yanga ni platform kubwa kwa wachezaji, hicyo nitapambana sana,” amesema Konkoni.

Mashabiki wengi wa Yanga wanatamani mchezaji huyo awe na uwezo kama Fiston Mayele ambaye ameondoka na kuacha alama kubwa klabuni hapo ambapo kwa misimu miwili amefunga mabao 54 na kuisadia timu yake kubeba mataji 6 ya ikiwemo Ligi Kuu mara mbili na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

SOMA NA HII  BAADA YA KUPITIA MAGUMU....RONALDO AWEKA REKODI MPYA ULAYA...APIGA GOLI LA 700 MAN UTD WAKIOSHA NYOTA ....