Home Habari za michezo SIMBA, YANGA VICHEKO TU KABLA YA KARIAKOO DABI

SIMBA, YANGA VICHEKO TU KABLA YA KARIAKOO DABI

KABLA ya mchezo wa Kariakoo Dabi itakayopigwa jijini hapa vikosi vyote viwili vimepokea taarifa njema ambazo zitawafanya watabasamu kwa kuongeza kitu kwao.

Tuanze na Simba wao watampokea kiungo Clatous Chama ambaye atarejea uwanjani kucheza mechi yake ya kwanza baada ya kusimamishwa msimu uliopita kwa mechi tatu.

Chama alisimamishwa baada ya kumkanyanga aliyekuwa kiungo wa Ruvu Shooting Abal Kassim Suleiman katika mchezo wa msimu uliopita ambao Wekundu hao walishinda mabao 3-0.

Chama hakupewa kadi nyekundu ambapo adhabu yake ilitoka kwa Kamati ya Usimamizi wa Ligi na sasa amemaliza adhabu hiyo kufuatia kukosa mechi hizo kati ya Polisi Tanzania, Coastal Union za msimu uliopita ambapo msimu huu wakaikosa ile juzi dhidi ya Singida Fountain Gate na sasa atakuwa tayari kucheza mchezo wa watani.

Yanga nao winga, Jesus Moloko atarejea kwenye kikosi hicho akitoka kutumikia adhabu kama hiyo aliyoipata msimu uliopita walipokutana na Mbeya City ambapo tayari alishazikosa mechi tatu dhidi ya Prisons na Azam za msimu uliopita ikiwamo fainmali ya ASFC kisha mechi ya mwisho ni ile ya ufunguzi wa Ngao dhidi ya Azam.

Kurejea kwa wachezaji hao kutakwenda kuzinufaisha timu zao ambapo kwa Simba atarejea Chama ambaye ni mmoja wa wachezaji tegemeo anayeongeza ubunifu kutoka katikati ya uwanja.

Yanga nao watampokea Moloko ambaye ni mmoja wa wachezaji wao tegemezi wakati huu ambao hawana uhakika kama winga wao mpya Mahaltse Makudubela ‘Skudu’ kama atakuwa tayari kwa mchezo huo ujao kufuatia kuumia mechi ya kwanza.

SOMA NA HII  BANGALA KUIKOSA YANGA ISHU IKO HIVI