Home Habari za michezo GAMONDI AFANYA KILA KITU MAPEMA SANA

GAMONDI AFANYA KILA KITU MAPEMA SANA

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi anataka kufanya biashara yake mapema baadaye aje kupiga mahesabu kama ataingia hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Maana yake wachezaji watakutana na mechi ngumu zaidi lakini pia kutakuwa na kusafiri kwenda kucheza mechi ngumu mfano labra na Wydad Casablanca umbali mrefu na kurudi nyumbani unatakiwa asafiri kwenda Kigoma kucheza na Mashujaa FC na baadhi ya nyota muhimu ndani ya kikosi utakuwa unewatumia.

Kwa hiyo kiufundi inapelekea kutopata matokeo mazuri au ushindi mnono kama ambavyo wanafanya sasa sababu ya uchovu.

Mfano mzuri msimu uliopita Yanga alitoka kucheza mechi ngumu Tunisia baada ya kurudi akasafiri mpaka Mwanza kucheza dhidi ya Kagera Sugar Yanga alishinda kwa goli moja la Clemence Mzize lakini Kagera Sugar walicheza sana mpira nankutengeneza nafasi japo walishindwa kuzitumia.

Mpaka sasa yanga amecheza michezo mitatu ya ligi kuu dhidi ya KMC, JKT Tanzania pamoja na Namungo FC na michezo yote hii wamecheza nyumbani na kuibuka na ushindi.

Mpaka sasa wamefunga jumla ya magoli 11 katika michezo mitatu na hawajaruhusu goli lolote hiyo ni dalili nzuri kwa bingwa mtetezi kuwa kwenye kiwango Bora na akiongoza kukaa kileleni kwa idadi ya magoli mengi ya kufunga.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO THANK YOU ZA SIMBA, YANGA ZILIVYOGEUKA NA KUWA WELCOME