Home Habari za michezo GAMONDI HAJARIDHISHWA NA NAMUNGO ISHU IKO HIVI

GAMONDI HAJARIDHISHWA NA NAMUNGO ISHU IKO HIVI

Habari za Yanga leo

Ushindi wa bao 1-0 ambao wameupata Young Africans dhidi ya Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara juzi Jumatano (Septamba 20) haujamtosha Kocha Miguel Gamondi ambaye amewageukia wachezaji wake kutokana na kushindwa kutumia nafasi nyingi za mabao walizozitengeneza.

Young Africans katika michezo miwili iliyopita ya ligi walifanikiwa kufunga mabao 10 kwa kushinda kila mchezo mabao 5-0 dhidi ya JKT Tanzania na KMC huku juzi wakipata ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya Namungo.

Kocha Gamondi amesema kuwa: Tumefurahi kwa kuwa tumefanikiwa kupata alama tatu na hilo ndiyo jambo muhimu zaidi kama timu kuhakikisha kuwa tunapata matokeo ya ushindi kwanza kuliko jambo lingine.

Ukiniuliza kama kocha tathmini yangu ya mchezo, basi nitakwambia kuwa wachezaji wangu walicheza vyema kimbinu lakini changamoto ambayo ilikuwa kwetu basi ni kushindwa kutumia nafasi nyingi ambazo tulizitengeneza.

Nacho: Bellingham alizaliwa kuitumikia Real Madrid “Kama timu na wachezaji kwa ujumla tunatakiwa kwenda kuboresha hili, wao wenyewe wanafahamu kwa kuwa hata wengine wameona ni kwa kiasi gani tulitengeneza nafasi nyingi za wazi ambazo zingeamua mechi yetu mapema zaidi.”

SOMA NA HII  MUDATHIR AWEKA SIRI ZA GAMONDI HADHARANI