Home Habari za michezo MBABE WA YANGA AFUNGUKA KILICHOMUONDOA IHEFU

MBABE WA YANGA AFUNGUKA KILICHOMUONDOA IHEFU

kocha ihefu

Saa chache baada ya klabu ya Ihefu kutangaza kuachana na kocha wake Zuberi Katwila mwenyewe amefunguka juu ya uamuzi huo akisema ameamua kuachana salama na klabu hiyo.

Katwila amesema kuondoka kwake Ihefu hakuna maana kwamba amefukuzwa kwa lolote akisema hayo ni makubaliano aliyofikia na mabosi wa klabu hiyo akitaka wapate changamoto mpya kutoka kwa makocha wengine watakaoendeleza pale alipoishia.

Kocha huyo ambaye ni kiungo wa zamani wa Mtibwa Sugar amesema wala hana shida na Ihefu katika makubaliano ambayo wamekubaliana kwenye kuachana akiweka wazi kwamba sasa anataka kutafuta changamoto mpya ya maisha yake ya ukocha.

“Hakuna baya lolote nadhani mnaona sehemu ambayo timu ilipo, ipo katikati ya msimamo na hatukuwa na mwendo mbaya sana ukizingatia ligi bado ni mbichi kabisa, nimekubaliana na viongozi wangu kwamba watafute kocha mpya na mimi nitafute changamoto mpya,”amesema Katwila.

“Sisi makocha maisha yetu yako hivyo kuna wakati hutakiwi kusubiri kuona unafukuzwa kama unaona kuna nafasi ya kufanya maamuzi mkiwa pamoja na klabu kwa maelewano mazuri mnafanya hivyo.

“Nimewaambia viongozi wangu wa Ihefu ukiacha kuwashukuru kwa imani yao kwangu lakini Ihefu itabaki kuwa klabu yangu kando ya mtibwa Sugar iliyonilea kama mchezaji na mpaka kuwa kocha, nawatakiwa kila la kheri wapate kocha bora zaidi yangu ili aendelezi nilipoishia.

Aidha Katwila akizungumzia taarifa za kutakiwa na Singida Big Stars amesema hawezi kuzuia taarifa za yeye kutakiwa na klabu zingine kwa kuwa kuondoka kwake Ihefu hakujamfanya kuachana na taaluma yake ya ukocha.

“Mimi nimeondoka Ihefu sijaachana na ukocha, watu wakisema na kwenda timu nyingine nafikiri siwezi kuwazuia kama kuna timu nitakwenda itajulikana tu.”

SOMA NA HII  HUYU AZIZI KI MNAEMUONA NI ASILIMIA 40 TU