Home Habari za michezo ROBERTINHO AFURAHISHWA NA MASTAA HAWA MECHI YA JANA

ROBERTINHO AFURAHISHWA NA MASTAA HAWA MECHI YA JANA

Habari za Simba

Kocha wa Simba Oliveira Robertinho amefurahishwa na namna ambavyo wachezaji wake walipambana jana licha ya kuondolewa kwenye michuano.

Simba jana ilikuwa mgeni wa Al Ahly ya Misri katika mchezo wa marudiano wa African Football League na kutoka sare ya bao 1-1 na kufanya matokeo ya jumla kuwa 3-3 na kuondolewa kwa kanuni ya bao la ugenini.

Akizungumza mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wakitokea Misri amesema, vijana wake wote wanastahili hongera kwa namna ambayo waliipambania timu na nchi kwa ujumla.

Amesema hata wapinzani wao hawakuamini walichokutana nacho lakini ndio mpira ulivyo ilitakiwa apatikane mshindi katika mchezo huo.

Aidha Robertinho amewapongeza zaidi Sadio Kanoute, Jean Baleke na Fabrice Ngoma kwa namna walivyocheza.

Amesema Ngoma na Kanoute walionyesha kitu cha ziada ambacho kilimkosha kutokana na utulivu mkubwa waliokuwa nao.

“Ni wachezaji wote wamepigana kuhakikisha Simba inasonga mbele lakini matokeo hayakuwa upande wetu, nawapongeza sana tunaangalia michezo ijayo maisha yaendelee,”anasema.

Amesema hakuna asiyefahamu ubora wa Al Ahly, kitendo cha kutoa sare kwao ni jambo kubwa na la kujivunia.

“Huko nyuma timu zilikuwa zikifungwa mabao mengi ugenini lakini Simba imepata sare tena na timu kwa kama hiyo, hayakuwa malengo lakini tulichokipata tunamshukuru Mungu,”

Sasa Simba inatakiwa kujipanga na kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ihefu Jumamosi.

SOMA NA HII  NAMUNGO WATUMA UJUMBE HUU KWA AZAM FC