Home Habari za michezo UNATAKA KUISHUHUDIA SIMBA VS AL AHLY VIINGILIO HIVI HAPA

UNATAKA KUISHUHUDIA SIMBA VS AL AHLY VIINGILIO HIVI HAPA

Simba vs Al Ahly

Simba imetangaza viingilio vya mchezo wao dhidi ya Al Ahly ya Misri wakisema kiingilio cha chini kuona mchezo huo kitakuwa ni sh 7,000 tu.

Msemaji wa Simba Ahmed Ally, amesema wameamua kuweka kiingilio hicho cha chini ili kuhakikisha mashabiki wao wanaujaza uwanja huo katika mchezo wa African Football league dhidi ya Al Ahly ya Misri utakaopigwa Oktoba 20, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mbali na kiingilio hicho cha chini vingine viti vya rangi ya machungwa vitakuwa ni sh 10,000, VIP C SH 30,000, VIP B sh 40,000 wakati tiketi za Platnium zitauzwa kwa sh 200,000.

Ally ameongeza kuwa kwenye mchezo huo hakutakuwa na tiketi za jukwaa kuu kutokana na eneo hilo litakaliwa na wageni maalumu kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa(FIFA),Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na wageni maalumu wa serikali.

“Tumeweka viingilio hivi ili kuhakikisha mashabiki wa Simba tunaujaza huu uwanja, ni heshima kwa klabu yetu na Taifa kwa kuchaguliwa mechi ya ufunguzi kuchezwa hapa nchini,amesema Ally.

“Tunatakiwa kujaa kama ambavyo tunaujaza uwanja tunapokuwa kwenye siku ya Simba, itakuwa aibu kwetu kama mchezo kama huu unaozihusisha klabu nane tu bora Afrika utachezwa hapa nchini huku uwanja ukiwa mtupu.”

SOMA NA HII  ISHU YA BILIONI 20 ZA MO NA KINGWANGALLA IMEFIKIA HAPA