Home Habari za michezo YANGA SASA WAWATAMANI AL AHLY BAADA YA SIMBA KUSHINDWA KUTAMBA

YANGA SASA WAWATAMANI AL AHLY BAADA YA SIMBA KUSHINDWA KUTAMBA

Habari za Yanga

UONGOZI wa Yanga, umesema kuwa, umetumia mchezo wa Simba kuwasoma wapinzani wao, Al Ahly ambao watakutana katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Yanga na Al Ahly wapo Kundi D katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu sambamba na timu za CR Beluoizdad ya Algeria na Madeama kutoka Ghana.

Katika michezo miwili ambayo Al Ahly imecheza dhidi ya Simba msimu huu kwenye michuano ya African Football League, yote imemalizika kwa sare. Ilianza 2-2 jiini Dar, kisha 1-1 kule Misri, lakini timu hiyo imefuzu nusu fainali kwa bao la ugenini.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema: “Tumefanikiwa kuwaona wapinzani wetu katika michezo miwili, kikubwa ni sisi sasa kujipanga kuhakikisha tunapata matokeo mazuri mbele yao.

“Yanga tumejipanga haswa na tutawashangaza, safari hii malengo yetu ni makubwa. Tumewasoma wapinzani wetu vyema, hivyo waleteni tuwaoneshe.

“Yanga tupo tayari kuwakabili Al Ahly, tunaamini sisi tuna timu nzuri ya kwenda kupambana nao, kwa sasa tunaelekeza nguvu katika michezo ya ligi iliyo mbele yetu,” alisema kiongozi huyo.

Mechi ya kwanza kati ya Yanga na Al Ahly inatarajiwa kufanyika kati ya Disemba 1 Yanga wakianza nyumbani huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kufanyika kati ya Machi 24 ukiwa mchezo wa mwisho wa kundi D.

Yanga itacheza dhidi ya Al Ahly kati ya Desemba 1 na 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, ukiwa ni mchezo wa pili wa Kundi D katika michuano hiyo baada ya kumalizana na CR Beluoizdad.

SOMA NA HII  HATIMAYE YANGA WAFUNGUKA...ISHU YA FEISAL SALUM "FEI TOTO"...WAMEZUNGUMZA HAYA