Home Habari za michezo KUHUSU BANGO LA 5G LA YANGA….SIMBA WAAMUA KUCHUKUA HATUA HIZI MAPEMAA…

KUHUSU BANGO LA 5G LA YANGA….SIMBA WAAMUA KUCHUKUA HATUA HIZI MAPEMAA…

Habari za Yanga SC

Kuhusu mabango ya Yanga ambayo yamewekwa sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam yakionyesha matokeo ya kuifunga Simba mabao 5-1, uongozi wa Simba umetoa kauli.

Meneja wa Habari wa Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wameyaona na mabango na maoni kutoka kwa watu mbalimbali kuhusu mtazamo wao wa kisheria.

“Niseme Simba ina idara ya sheria hili wameliona na wenyewe wanalitazama kwa jicho lao waone kama kuna hoja kama hakuna tuwaache wafanye wanachofanya,” amesema Ahmed na kuongeza;

“Narudia hiki chote kinachoendelea tumesababisha wenyewe, sisi wenyewe ndiyo tunaweza kubadilisha hii kadhia hasa wachezaji wa Simba wakiona wasema mimi nimesababisha bango kubandikwa ili wakati ujao afanye linalowezekana isijirudie,”

Ahmed amesema ana imani na wachezaji kuwa Novemba 25 watafanya makubwa timu hiyo itakapocheza mechi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Asec Mimosas na kuipigania Simba kwakuwa timu ikipata matokeo mazuri watapunguza machungu makubwa wanayopita hivi sasa.

“Ni muhimu wajue pale hawachezi tu kwa ajili yao bali kwa ajili ya Simba. Sisi tutaenda kutimiza wajibu wa kushangilia, na wao watupe furaha ili turejeshe hali yetu ya kutamba. Tunawambia hivyo kwa niaba ya mgeni rasmi, mashabiki wa Simba,” amesema Ahmed

Kuhusu hali ya majeruhi Ahmed amesema; “Kibu tayari amerudi, Kanoute anaendelea vizuri, Isra Mwenda tayari amerudi mazoezini na Kramo bado anaendelea kuuguza jeraha. Akipona atarudi kutumikia klabu,”

SOMA NA HII  YANGA TIMU YA KWANZA KULETA KOMBE LA CAF..."WANANCHI MSIHOFU TUNABEBA...HAKUNA WA KUTUZUIA