Home Habari za michezo GAMONDI AL AHLY WEPESI TU HAKUNA PRESHA

GAMONDI AL AHLY WEPESI TU HAKUNA PRESHA

Habari za Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi, amesema hana presha kuelekea mchezo ujao dhidi ya Al Ahly, huku akibainisha kwamba utakuwa mzuri kwa Wananchi.

Gamondi ametoa kauli hiyo kwa kujiamini, kisha akabainisha kwamba, atakuwa na muda mwingi wa kuiandaa timu kupata matokeo mazuri.

Mchezo huo wa pili wa Kundi D katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, umepangwa kuchezwa Desemba 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

“Sina presha, mechi ya Dar es Salaam dhidi Ahly itakuwa mechi nzuri kwa Wananchi kwani baada ya mchezo wa kwanza ugenini, nitakuwa na muda wa kutosha wa kuiandaa timu,” alisema Gamondi.

SOMA NA HII  GAMONDI APEWA MAAGIZO HAYA KUHUSU AL MAREKH YA SUDAN