Home Habari za michezo MADEAMA MAPEMA SANA HUKU WAKIMKOSA MWAMBA HUYU DHIDI YA YANGA

MADEAMA MAPEMA SANA HUKU WAKIMKOSA MWAMBA HUYU DHIDI YA YANGA

Habari za Yanga

Kikosi cha Medeama ya Ghana kinatarajiwa kuja nchini Jumapili Desemba 17 kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa raundi ya nne wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam utakaopigwa Jumatano Desemba 20, kuanzia saa 10:00 jioni.

Katika mchezo huo, mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Ghana, itamkosa beki wao wa kati, Nurudeen Abdulai (24), kutokana na majeraha ya bega baada ya kuumia kwenye mchezo wa sare ya bao 1-1 dhidi ya Yanga, jijini Kumasi kwenye Uwanja wa Baba Yara.

Beki huyo amekuwa mhimili mkubwa akiisaidia timu hiyo kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo na kukosekana kwake kunaweza kukaathiri safu yao ya beki, ingawa kocha wa timu hiyo, Evans Adotey licha ya kueleza kusikitishwa kwake na kumpoteza Abdulai kwenye mchezo huo, ana imani na uwezo wa timu yake kupata ushindi na ana wachezaji wazuri kama kipa Felix Kyei na mshambuliaji Jonathan Sowah.

Katika mchezo wa kwanza, Medeama ndiyo iliyotangulia kupata bao dakika ya 27 kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Sowah baada ya beki wa Yanga, Dickson Job kumfanyia madhambi, Derrick Fordjour eneo la hatari.

Yanga ilijibu mapigo na kusawazisha bao hilo kupitia kwa nyota wa kikosi hicho, Pacome Zouzoua dakika ya 36 likiwa ni la pili kwake katika mashindano haya baada ya kufunga pia mechi iliyopita dhidi ya Al Ahly katika sare ya 1-1.

Timu zote zinakwenda kukutana zikiwa zimepania kuibuka na ushindi, huku Medeama ikitaka kuendeleza kiwango chao cha kuvutia kwenye michuano hiyo hadi sasa na Yanga SC ikihitaji kupata ushindi nyumbani ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye kundi hilo D.

Medeama iko nafasi ya tatu na pointi nne sawa CR Belouizdad ya Algeria, huku bingwa mtetezi wa michuano hiyo, Al Ahly ikiongoza kundi ikiwa na pointi tano na Yanga SC ikishika mkia na pointi mbili na kila timu ikiwa bado na nafasi ya kusonga mbele hatua ya robo fainali kama zitatumia vyema michezo yao.

SOMA NA HII  CHAMA APIGA MKWARA MZITO...KOCHA BIASHARA 'AGWAYA' TIZI LA SIMBA...GSM NA TFF WAENDELEA KUSOMANA...