Home Entertainment TECNO YAGUSA HISIA: MCHEZO WA HISANI WACHOCHEA HAMASA YA KUBORESHA VIWANJA VYA...

TECNO YAGUSA HISIA: MCHEZO WA HISANI WACHOCHEA HAMASA YA KUBORESHA VIWANJA VYA JAMII BARANI AFRIKA

Tecno

Kama mdhamini rasmi wa Kombe la  (AFCON) Afrika nchini Côte d’Ivoire, kampuni ya teknolojia , TECNO iliandaa mechi ya hisani iliyojaa nyota magwiji wa mpira wa miguu Africa siku ya pili ya sherehe ya ufunguzi.

Mechi hiyo ilishirikisha Katibu Mkuu wa CAF, Véron Mosengo-Omba, wachezaji maarufu wa mpira akiwemo Jay-Jay Okocha, El Hadji Diouf, Asamoah Gyan, Dennis Oliech, na Erick Otieno, waliyoonyesha ushirikiano wao kwa michezo na maendeleo ya jamii.

TecnoKabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki, TECNO ilitangaza mpango wa kufadhili matengenezo ya viwanja 100 vya mpira vya jamii zote Afrika ndani ya miaka mitano ijayo.

Mpango huu unalenga kuhamasisha ushiriki wa vijana, kukuza maisha yenye afya, na kuhakikisha upatikanaji wa viwanja bora vya michezo katika jamii zisizopewa kipaumbele.

Meneja Mkuu wa TECNO, Jack Guo, alisema kwa hamasa, “Tumeanzisha safari ya kuzitia mwangaza ndoto zisizohesabika kwa kuboresha viwanja 100 kote Afrika,” akisisitiza nguvu ya kubadilisha ya mpango wa TECNO.

TecnoTaylan Tankpinou, mvulana wa miaka 10, aliongeza, “Asante kwa TECNO, tunajenga maeneo bora ya kuchezea na kukua!

Ili kuhamasisha zaidi, TECNO ilitangaza kwamba kwa kila goli lililofungwa katika mchezo huo liligharimu, dola $10,000 ambazo zingechangiwa kwenye kampeni hiyo.

Mchezo ulimalizika na TECNO kuchangia dola $50,000 zaidi kwa mradi huo. Ahadi hii ilifanya kila goli kuwa shangwe si tu kwa wachezaji bali pia kwa vizazi vijavyo ambavyo vitafaidika na miundombinu bora.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA YANGA NA AZAM ZINAZIDI KUTAMBULISHA 'VIFAA VIPYA'...SIMBA WAIBUKA NA KUJIBU MAPIGO KWA STAILI HII...