Home Habari za michezo NTIBAZONKIZA KASALIMIKA SIMBA…?, UKWELI WOTE HUU HAPA….BENCHIKHA ANAHUSIKA…

NTIBAZONKIZA KASALIMIKA SIMBA…?, UKWELI WOTE HUU HAPA….BENCHIKHA ANAHUSIKA…

Habari za Simba leo

Imefahamika kuwa Kocha Mkuu wa Simba SC, Mualgeria Abdelhak Benchikha ndiye aliyenusuru panga kwa kiungo wake mshambuliaji, Said Ntibanzokiza ‘Saido’ kuendelea kubakia Msimbazi.

Awali kiungo huyo alikuwepo katika mipango ya kuachwa katika usajili huu wa dirisha uliofungwa usiku wa kuamkia jana Jumanne (Januari 16), baada ya kuwepo mvutano wa kimaslahi ya mkataba.

Kiungo huyo aligomea kusaini mkataba wa mwaka mmoja aliowekewa mezani na mabosi zake huku akishinikiza kupewa miwili ambao waajili waligomea na kubariki aondoke kabla ya Benchinka kumbakiza.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, imefahamika kuwa Mkuu wa Benchi la Ufundi la timu hiyo, Benchikha ndiye aliyewashawishi viongozi kumbakiza kiungo huyo kwa kumpa mkataba wa miaka miwili wenye masharti.

Mtoa taarifa huyo amesema kuwa suala hilo la Saido liliwagawa viongozi kabla ya kocha huyo kupendekeza aongezewe mkataba huo wa miaka miwili akiamini, ataongeza kitu katika mashindano yaliyokuwepo mbele yao.

Ameongeza kuwa Benchikha tangu ametua nchini anafuatilia kwa karibu kiwango cha Saido ambacho kimemvutia na kupelekea kumbakisha hapo Simba SC, licha ya baadhi ya viongozi kupendekeza kuachana naye.

“Haikuwa kazi rahisi Saido kubakia Simba SC, ni baada ya kuleta mvutano mkubwa hadi kumbakisha katika usajili huu wa dirisha uliofunga usiku wa kuamkia jana Jumanne.

“Na kama siyo kocha Benchikha kuwasilisha ripoti ya usajili ambayo ilimuonyesha Saido abakie hapo, basi jina lake lingekatwa kutokana na viongozi kutomuhitaji.

“Kikubwa walikuwa wakibishana katika ukomo wa mkataba ambaye yeye aligomea mkataba wa mwaka mmoja na kutaka miwili ambayo waligomea viongozi kutokana na umri mkubwa alionao,” amesema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally kuzungumzia hilo alisema kuwa “Hilo suala la kiufundi zaidi, lipo chini ya kocha wetu Benchikha, lakini fahamu kuwa Saido bado mchezaji wa Simba SC.”

SOMA NA HII  GAMONDI: AFUNGUKA KUHUSU WACHEZAJI WAKE KUFUNGA MAGOLI MATANO.... SIO LENGO LETU...AFUNGUKA HAYA