Home Habari za michezo KUHUSU KUSUGUA BENCHI YANGA…SKUDU AVUNJA UKIMYA…AGUSIA KUKATA TAMAA…

KUHUSU KUSUGUA BENCHI YANGA…SKUDU AVUNJA UKIMYA…AGUSIA KUKATA TAMAA…

Habari za Yanga SC

Kiungo Mshambuliaji ‘WINGA’ wa Young Africans, Mahlatse Makudubela ‘Skudu’ amesema hajakata tamaa na anaendelea kupambana kusaka namba katika kikosi cha timu kinachoendelea kusaka pointi muhimu ili kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Skudu, raia wa Afrika Kusini ameshindwa kupata namba katika kikosi cha timu hiyo kinachonolewa Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Skudu amesema ameshindwa kupata nafasi ndani ya kikosi cha kwanza kwa sababu ya ushindani uliopo, lakini kamwe hawezi kukata tamaa na anaamini ataisaidia timu kila atakapopata nafasi ya kucheza.

Nitaendelea kujituma katika mazoezi na ninaamini ninatakiwa kuonyesha kitu kila nafasi ya kucheza nitakayopewa na kocha, bado nina nafasi kwenye timu, wakati ukifika nitaonyesha ubora wangu,” amesema Skudu.

Ameongeza anaimani na kiwango chake bado kipo vizuri kwa kusaidia Young Africans kufikia malengo yao kwenye mashindano ya ndani na yale ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika wanayoshiriki.

Amesema morali ya wachezaji wa Young Africans iko juu kwa sababu wanajipanga kuwapa furaha wanachama na mashabiki wao kila wanapocheza.

“Ni kweli ushindani wa namba ni mkubwa, kikubwa nitapambana kuhakikisha ninafanya vizuri na kusaidia Young Africans kupata matokeo chanya, ninaimani nitaonyesha kiwango kizuri kila ninapopata nafasi ya kucheza.

Mashabiki wa Young Africans wanapenda mpira jambo ambalo naliona ni zaidi ya familia kuichezea timu hii na niwaambie kuwa nitapambana kwa ajili ya kuyapata mafanikio makubwa zaidi na kuweka historia nyingine,” amesema Skudu.

Ameongeza anaendelea kuongeza juhudi kwenye uwanja wa mazoezi huku akisema bado mechi zilizobakia kukamilisha msimu ziko nyingi.

Usajili wa nyota huyo ulifanyika kwa mbwembwe na jezi namba sita aliyopewa ambayo awali ilivaliwa na kiungo, Feisal Salum ‘Fei Toto’, ilionekana itaipa faida kubwa Young Africans.

SOMA NA HII  BADO NI SIMBA, YANGA SASA NI KIGOMA UNAAMBIWA SIO POA