Pichani ni Carlos Sylvester [Mastermind], Agent wa wachezaji mbalimbali kwenye ligi yetu akiwa na viongozi wa Timu za Simba na Yanga.
Pale Yanga anawasimamia wachezaji wawili, Bakari Nondo
Mwamnyeto na Gift Mauya na Simba ana wachezaji wanne ambao ni Mzamiru Yassin, Kibu Denis, Mohamed Hussein na Hussein Kazi.
Kibu Denis, Mzamiru Yassin na Mwamnyeto mikataba yao inaelekea mwishoni, Carlos anafahamu huu ndio wakati wa kutengeneza pesa kupitia wateja wake.
Katika nyakati hizi ni rahisi sana kusikia Mwamnyeto anataka kwenda Simba na Kibu Denis anataka kwenda Yanga ilimradi tu ‘Mteja’ apate thamani anayoitaka Agent.
Iko hivi… Kwenye kujadili mkataba mpya wa Kibu Denis ni rahisi sana Simba kuulizia uwezekano wa kumpata Nondo na pia Yanga wanapojadili namna ya kuongeza mkataba wa Mauya ni rahisi kuulizia huduma ya Kibu, Zimbwe au Mzamiru. Hapa ndipo tetesi zinapozaliwa na kusambaa.