Home Habari za Simba Leo BAADA YA KUACHWA SIMBA…BOCCO APATA DILI KUBWA

BAADA YA KUACHWA SIMBA…BOCCO APATA DILI KUBWA

Habari za Simba

SIKU chache tu baada ya kupewa ‘Thank You’ na Simba, aliyekuwa nahodha wa timu hiyo, John Bocco amewasapraizi Wekundu wa Msimbazi wakati wenyewe wakijiandaa kumuaga rasmi.

Taarifa za ndani zinasema kwamba Bocco anayeshikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Ligi Kuu Bara akifunga mabao 154 katika misimu 16 akiipiku rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ aliyekuwa amefunga mabao 153 ndani ya misimu 13 amesajiliwa na JKT Tanzania kama kocha mchezaji.

Kabla ya kutua kwa maafannde hao wa JKT Tanzania John Bocco alikuwa ni kocha wa timu ya vijana ya Simba, hivyo suala la yeye kujiunga na Maafande hao inamaanisha hatokuwa tena sehemu ya benchi la ufundi la Simba.

John Bocco ndiye alikuwa ni mchezaji wa kwanza kabisa kupewa mkono wa kwaheri, lakini amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu sana, baada ya yeye mwenyewe kuomba kuachana na kucheza kutokana na kile kinachoelezwa ni umri mkubwa.

Awali walianza mashabiki kuhoji kiwango cha nohodha huyo, huku baadhi yao wakienda mbali sana na kusema umri wake mkubwa sio wa kuendelea kuichezea tena Simba.

Huenda ukawa unajiuliza John Bocco ni kwanini anaimbwa sana, je rekodi zake ndani ya uwanja zikoje? gwiji huyu hana namba mbaya kabisa ana rekodi nzuri tu licha ya kutundika daruga.

REKODI ZA JOHN BOCCO AKIWA SIMBA.

2017/2018 (14)

2018/2019 (16)

2019/2020 (9)

2020/2021 (16)

2021/2022 (3)

2022/2023 (10)

2023/2024 (2)

Jumla mabao 70

SOMA NA HII  LOMALISA APEWA THANK YOU YANGA...AMFUATA ZAHERA