Home Habari za Simba Leo WATATU KUBAKI SIMBA…12 KUPEWA THANK YOU AKIWEMO PUTIN.

WATATU KUBAKI SIMBA…12 KUPEWA THANK YOU AKIWEMO PUTIN.

Habari za Simba

MNYAMA Simba SC anafanya mabadiliko kimyakimya kwenye kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao, na mabadiliko makubwa yanaendelea kufuatia kushindwa kufanya vizuri katika misimu mitatu iliyopita.

Kwa mujibu wa Taarifa zilizotufikia kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya Simba ni kwamba klabu hiyo itabaki na wachezaji wake watatu tu wa kigeni kati ya 12 waliosajiliwa klabuni hapo.

Miongoni mwa watakaobaki ni Aubrin Kramo, ambaye alikosa msimu mzima uliopita kutokana na majeraha ya muda mrefu lakini sasa amepona kabisa na yuko tayari kukipiga.

Mbali na mabadiliko katika wachezaji wa kigeni, Simba SC imeanzisha mabadiliko miongoni mwa wachezaji wa ndani.

Nahodha wa klabu hiyo John Bocco, Kennedy Juma na Shaban Chilunda ni miongoni mwa waliopewa Thank You, huku Shomari Kapombe akiwa ameongeza mwaka mmoja zaidi. Wakati huo huo, Abdallah Hamis na Jimmson Mwanuke, ambao kwa sasa wako kwa mkopo Mtibwa Sugar, wanatarajiwa kuagwa timu hiyo, kwa mujibu wa habari za ndani.

Mabadiliko haya ya klabu yanaonyesha jitihada makini za uongozi kujenga upya kikosi, ikitambua haja ya kuanza upya wakati wakishukuru kwa mchango wa wachezaji muhimu kutoka kampeni za mafanikio za nyuma.

Baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu msimu uliopita, Simba SC tayari imetangaza kuachana na wachezaji watatu wa kigeni: Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’, Luis Miquissone, na Henock Inonga. Inonga amehamia FAR Rabat huko Morocco.

Mabadiliko zaidi yanatarajiwa, huku mchezaji wa muda mrefu Clatous Chama na wengine wakiripotiwa kuwa karibu kuondoka klabuni hapo ili kutoa nafasi kwa usajili mpya.

Wachezaji wa kimataifa waliobaki kama Kramo, Ayoub Lakred, Fabrice Ngoma, na Che Malone Fondoh wanatarajiwa kuendelea kubaki mitaa hiyo ya Msimbazi.

Vyanzo kutoka Simba SC vimehakikisha kuwa kiungo Sadio Kanoute ameamua kutoongeza mkataba mpya na yuko mbioni kuondoka. Klabu inaripotiwa kuwa katika mazungumzo ya mwisho kumchukua Augustine Okejepha kutoka Rivers United ya Nigeria ili kuziba pengo lililoachwa na Kanoute.

Mtu wa ndani wa klabu alisema, “Mkataba wa Kanoute umeisha na ameonyesha nia ya kuondoka. Tunaendelea kutafuta chaguo za kuimarisha kiungo chetu, na matangazo kuhusu mabadiliko haya yanakaribia.”

SOMA NA HII  KOCHA MPYA SIMBA HUYU HAPA...NI MMOROCCO MWENYE MBINU KALI UWANJANI...AHMED ALLY AFUNGUKA....