Home Habari za Simba Leo HENOCK INONGA ANAFOSI KUONDOKA… SIMBA WAWEKA KIGINGI

HENOCK INONGA ANAFOSI KUONDOKA… SIMBA WAWEKA KIGINGI

Habari za Simba Leo- Inonga kuondoka

Inaelezwa kwamba, Henock Inonga Baka amepata timu hivyo ameuambia Uongozi wa klabu hiyo, anahitaji kuondoka msimu huu, lakini Simba wamemueleza kwamba bado ana mkataba nao hivyo timu inayomhitaji awaambie waje kufanya biashara.

Kwa ufupi ni kwamba Simba inaonekana hawana mpango tena ya kuendelea na Henock Inonga kwa msimu ujao,  lakini hawataki kumuacha aondoke bure, wanahitaji kufanya biashara ya maana baada ya kitasa hicho   kuonesha kiwango kizuri sana kwenye mashindano ya AFCON huko Ivory Coast akiwa na timu yake ya Taifa ya DR Congo.

Kwa kutibitisha hilo, tayari Uongozi wa Lunyasi umeanza taratibu na mazunguzo na beki wa Namungo na timu ya taifa ya Burundi, Derick Mukombozi, ili awe mbadala wa Inonga endapo ataondoka.

Kama mazungumzo yao yataenda sawa, na kufikia makubaliano hayo, basi beki hilo litaungana na wachezaji wengine ambao tayari wameshasajiliwa kama Lameck Lawi beki wa Kushoto na Yusuph Kagoma Kiungo, Serge Pokou (Kiungo), Elie Mpanzu kama winga wa kushoto anayetumia miguu yote kupiga mashuti makali.

Kennedy Juma amekuwa mbadala wa Henock Inonga kwa mechi nyingi, lakini ana nafasi ndogo sana ya kucheza Simba msimu ujao, kwani tayari ameanza kufanya mazungumzo na klabu ya Tanga, Coastal Union ili kuongeza nguvu kwenye kombe la Shirikisho Afrika, ambapo mechi za hatua ya awali zitaanza katikati ya mwezi Agosti.

SOMA NA HII  JOHN BOCCO AKIWASHA SANA...SIMBA WAJITAFAKARI.