Home Habari za Usajili Yanga TETESI ZA USAJILI YANGA…LOBOTA ANUKIA…ANAJUA KUFUNGA

TETESI ZA USAJILI YANGA…LOBOTA ANUKIA…ANAJUA KUFUNGA

Habari za Yanga Leo

KLABU ya Yanga ipo kwenye mazungumzo ya karibuni zaidi na mshambuliaji wa klabu ya Ihefu Emmanuel Bola Lobota.

Lobota aliyejiunga na Ihefu katika dirisha dogo la msimu uliopita akitokea FC Saint Eloi Lupopo ya DR Congo amekuwa kwenye mawindo ya Yanga tangu mwanzoni mwa msimu uliopita.

Nyota huyo kabla ya kutua Ihefu, alishafanya mazungumzo na Yanga na Singida Fountain Gate, lakini baada ya mgawanyiko wa Singida FG ndipo akaibukia Ihefu ambayo inaelezwa imeshikilia dili la kujiunga na Yanga ili walete jembe jingine jipya.

Taarifa kutoka chanzo cha uhakika zinaeleza kwa tayari mshambuliaji huyo yupo hatua nzuri katika mazungumzo na Yanga na kama mambo yataenda sawa, basi msimu ujao atavaa jezi za Wananchi ambao wanashikilia mataji ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho kwa msimu wa tatu mfululizo.

Kupitia kwa Rais wa klabu hiyo Injinia Hersi Said alinukuliwa akisema kwamba msimu huu wamejipanga kufanya usajili mkubwa na mzuri, utakaoongeza ushindani kwenye kikosi cha wananchi.

Ikumbukwe kuwa Yanga itaiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa kwa msimu ujao 2024/25, hivyo suala la usajili ni jambo lisiloepukka,  ili kuwa na kikosi kipana na chenye ushindani.

Tayari  Uongozi wa Yanga chini ya Injinia Hersi umeshaanza mipango ya usajili na baadhi ya majina yapo mezani, kujadiliwa ikiwemo baadhi ya nyota wa kigeni akiwemo Emmanuel Lobota.

SOMA NA HII  SABABU 5 YANGA KUINGILIA DILI LA SIMBA KWA MWAMNYETO