Home Habari za Simba Leo MZEE DALALI, ALI KIBA WAITEKA MORO…SIMBA DAY MIKUMI

MZEE DALALI, ALI KIBA WAITEKA MORO…SIMBA DAY MIKUMI

Habari za Simba- Hassan Dalali

MWENYEKITI wa zamani wa Simba, Hassan Dalali na Msanii Mkubwa Afrika Ali  Kiba walikutana kwenye uzinduzi wa Simba Day Morogoro,  ambapo safari ya kwenda Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ikiendelea.

Mzee Hassan Dalali amesema miongoni mwa mambo ambayo anatamani kuona ni Mkoa wa Morogoro una uwanja mkubwa na wenye hadhi ya kimataifa ili timu hiyo ihamie hapo.

Mzee Hassan Dalali amesema hayo katika stendi ya zamani mjini humo muda mfupi baada ya msafara wa Simba kuwasili ukitokea Dar es Salaam kwa ajili ya kuzindua wiki ya Simba Day ikiwa ni pamoja na kutambulisha jezi za msimu ujao wa 2024/25  kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

Mwanzilishi huyo wa Simba Day amesema Morogoro timu yao  iliwahi kutangaza ubingwa mara mbili wakati akiwa kiongozi, hivyo ina historia nzuri na mkoa huo.

“Mjenge uwanja sasa Simba ibakie hapa Morogoro. Hapa ni nyumbani kwetu japo Simba ni ya kila sehemu. Leo tunazindua jezi, nawaomba wana Simba kila mmoja akanunue jezi tuujaze uwanja tukiwa na jezi zetu. Tofauti na zamani mwaka huu jezi zimetoka kabla ya Simba Day,” amesema.

“Jezi za awamu hii ni hatari tu kudadadeki… jamaa (Yanga) nawapa salamu. Mimi ndio mwanzilishi wa Simba Day ila tarehe 8 siku yetu halisi tunakutana na wale jamaa kazi wanayo. Tuna wachezaji hawalogeki. Tunaanza tarehe 3 katika siku yetu kabla ya wale mabwana nao kuona chamoto,” amesema mwenyekiti huyo wa zamani.

KIBA AITEKA MORO

Msanii wa Bongofleva, Alikiba ametambukishwa na Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally mjini Morogoro kuwa ndiye  mtumbuizaji kinara katika tamasha la 16 la Simba Day kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Semaji la CAF, kama ambavyo amekuwa akipenda kujiita Ahmed, alimtangaza Kiba akisema: “Mabibi na mabwana, nasema hivi Alikiba ndiye atakayetumbuiza Simba Day.”

Mara baada ya kutambulishwa Kiba alipanda jukwaa kuu akiwa na usaidizi wa mabaunsa na kuwasalimia mashabiki wa Simba ambao wamejitokeza katika stendi hiyo ya zamani.

“Kama kutakuwa na lolote wana Simba watafahamu, kwa sasa suala hilo lipo ngazi ya juu na limefika TFF, mbivu na mbichi zitajulikana hapo pande zote zitakapokutana,” alisema Ahmed.

SOMA NA HII  SIMBA YACHAGULIWA KUCHEZA LIGI HII...NI LIGI YA WAFALME TU...YANGA YAPIGWA CHINI