Home Habari za Simba Leo AAGY SIMBA ALIA NA ADHABU ALIYOPEWA…NINAKOSA HAKI…SIKO HURU

AAGY SIMBA ALIA NA ADHABU ALIYOPEWA…NINAKOSA HAKI…SIKO HURU

Habari za Simba- Aggy Simba

MWANACHAMA wa Mnyama Simba Agnes Malkiad maarufu Aggy Simba, amelalamikia kitendo cha Sekretarieti ya Klabu hiyo kumfungia kujihusisha na masuala yanohusu klabu hiyo akitaka afikishwe katika kamati ya maadili kwaajili ya kuwasilisha utetezi wake.

Akizungumzia kufungiwa kwake Aggy Simba amesema barua aliyopewa na sekretarieti hiyo inasema amefungiwa kwa kosa la kuitisha mkutano kinyume cha taratibu na kuchochea migogoro ndani ya klabu jambo ambalo anadai siyo kweli.

“Ninakosa haki kama mwanachama wa Simba kwasababu barua inasema tutaitwa kwenye kamati ya maadili na hatujaitwa mpaka sasa ili nikasomewe mashtaka yangu na mimi niweze kusikilizwa.

“Siruhusiwi kujishughulisha na masuala ya klabu kama yapi? ninakosa haki ya kuwa huru. Kurushwa katika mitandao ya kijamii ya Klabu ya Simba kwamba nimefanya hayo mambo ni kulichafua jina langu” amelalamika

Aggy Simba alisema barua inaeleza ataitwa katika kamati ya maadili lakini mpaka sasa bado hajaitwa na hajui nini kinakwamisha kupata haki yake.

Aggy Simba, ambaye mbali na kuwa mwanachama wa simba pia ni mshabiki kindakindaki wa timu hiyo anashahuku ya kurejea kuendelea kuisapoti timu yake huku akisifu kitendo Mohamed Dewji Maarufu ‘Mo’ kurejea katika nafasi ya Uenyekiti wa Bodi na kueleza kitendo hicho kitaipatia timu hiyo matokeo chanya katika msimu ujao.

Sababu ya kufungiiwa ni kuhamasisha mkutano wa Wananchama bila kinyume na utaratibu, mkutano huolengo lilikuwa ni Kuwakutanisha Wanachama na kutoa maoni yao juu ya uatawala wa Mwenyekiti Mangungu na Salim Try Again ndani ya Simba.

Aggy Simba hayupo peke yake kwenye kifungo hicho, bali kuna mwenzake mmoja anaitwa Dkt Mohammed aliyekuwa msemaji wa Tawi la VIP B nae amefungiwa.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSHINDWA KUWASAJILI AZIZ KI NA ADEBAYOR...AHMED ALLY AIBUKA NA HILI...ADAI HAWAKUWA NA HADHI...