Home Habari za Simba ALI  KAMWE ATOA KAULI  TATA KWA SIMBA…HALI IMEBADILIKA MSIMBAZI

ALI  KAMWE ATOA KAULI  TATA KWA SIMBA…HALI IMEBADILIKA MSIMBAZI

Habari za Simba leo

Ali Kamwe Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga amesema Agosti 8 wataitumia ‘kushona’ midomo ya wale wanaoamini kuna timu zimekaribia daraja la Yanga baada ya usajili wa dirisha hili.

Mnamo Agosti 8, Yanga itachuana na Simba katika mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akizungumza muda mfupi baada ya kutua Afrika Kusini ambako Yanga itashiriki michuano maalum ya Mpumalanga, Kamwe amesema baada ya maandalizi na mechi watakazocheza katika pre-season hapo Afrika Kusini, anaamini watarejea nchini wakiwa tayari kuwapa furaha mashabiki wao.

“Agosti 8 ni siku ya kuwashona midomo watu! Unajua kuna watu wanaamini timu zao zimekaribia daraja la Yanga hivyo siku hiyo tutakwenda kuwaonyesha Yanga iko katika daraja lake tofauti,” alitamba Kamwe.

Katika hatua nyingine, Kamwe amesema wanatarajia mchezo dhidi ya Augusburg utakaopigwa kesho huko Mpumalanga utakuwa mgumu licha ya kuwa ni mechi ya pre-season.

Yanga iltua Afrika Kusini jana usiku na kupokelewa mashabiki wengi katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo.

Yanga na Augusburg zilikutana uwanja wa ndege lakini kilichowashangaza Wajerumani hao ni msisimko mkubwa wa mashabiki kuonakena upande wa Yanga kuliko wao licha ya kuwa ni timu inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani.

Kamwe amesema amekuwa na mawasiliano na Afisa Habari wa Augusburg ambaye amekiri kushangazwa na hamasa kubwa ya mashabiki wa Yanga ambao kama kawaida yao wamevamia kurasa za mitandao ya kijamii za klabu hiyo ‘kuwapiga mkwara’.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AONA ISIWE TABU AONGEZA BEKI MWINGINE